BAADA YA MBUNGE WA CCM KUTANGAZWA MSHINDI NYAMAGANA MWANZA, WENJE AMEYAONGEA HAYA MBELE YA WAANDISHI WA HABARI LEO



Jimbo la Nyamagana Mwanza ambalo lilikuwa chini ya mbuge Ezekiel Wenje lipo kwenye headlines sasa hivi ambapo matokeo ya uchaguzi mkuu 2015 Stanslaus Mabula aliyekua Meya wa Mwanza, yamemtangaza mshindi.

Baada ya ushindi huo wa Mabula, Ezekiel Wenje ameyazungumza haya mbele ya Waandishi wa habari >>> ‘Tulikubaliana kwamba wale vijana waliokua wanafanya kazi ya kuingiza yale matokeo waende kuchukua wino waje waweke palepale ofisini waje waprint ili kila mgombea apate matokeo yote walivyoingiza kwa kila kituo na kila kata alafu tujumlishe jumla tupate mshindi‘

‘Wale vijana walivyoondoka kwenda kuleta wino, aliyesimamia uchaguzi akasimama akasema hakuna haja ya kusubiri… wakaja na matokeo ambayo sio hata kwenye ile list rasmi, kuna vitu vingine waliandika pembeni ambavyo tayari walishasave ndio wakafungua… pia wiki mbili kabla ya uchaguzi walimuhamisha mkurugenzi wa jiji la Mwanza Hassan Ida na kumpeleka TAMISEMI, kanuni inasema mtu yeyote anaesimamia uchaguzi hatoamishwa mpaka uchaguzi uishe‘ – Wenje


Stanslaus Mabula.

‘Sheria inataka kura ikishapigwa pale wanapojumlisha matokeo wakishamaliza kujumlisha yale matokeo yanatakiwa kuwekwa kwenye fomu (Namba 21 kwa kura za Mbunge) lakini kwa masikitiko makubwa kuna kata nyingi sanasana kata ya Igoma na Kishiri Mawakala wetu walinyimwa hizo fomu‘ – Ezekiel Wenje.

Kwenye sentensi ya mwisho Ezekiel Wenje ametangaza kwenda Mahakamani kupinga matokeo hayo na kusema >>> ‘tunajiandaa na Mawakili wetu tunakutana nao ili waandae kesi, ushahidi tunao‘
 Chanzo-Millardayo.com

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527