Hapa ni katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambako leo kumefanyika mkutano wa tume ya taifa ya uchaguzi(NEC) na viongozi wa vyama vya siasa mkoani Shinyanga kujadili mambo mbalimbali yanayohusiana na uchaguzi mkuu ujao ikiwemo suala la amani...Malunde1 blog ilikuwepo eneo la tukio...Mwandishi wetu Kadama Malunde ametuletea picha 25....Angalia hapa chini...
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha akizungumza wakati wa mkutano huo ambapo aliwataka viongozi wa siasa kuacha kupotosha wafuasi wao kwa kuwaaminisha kuwa lazima walinde kura nje ya mita 200.
Kamanda Kamugisha ameongeza kuwa hakuna sehemu yoyote katika sheria inayosema wapiga kura wasimame nje ya mita 200 kutoka kwenye kituo cha kupigia kura wala kulinda kura,hivyo kuomba kila chama cha siasa kitumie wanasheria wake kutafsiri sheria vizuri badala ya kupotosha wananchi.Kamugisha alihamasisha watanzania kulinda amani ya nchi kwani ni kitu cha pekee katika taifa lolote
Mratibu wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga Projestus Rutabanzibwa akizungumza wakati wa mkutano huo wa tume ya taifa ya uchaguzi na viongozi wa vyama vya siasa mkoa wa Shinyanga
Mkutano unaendelea
Viongozi wa vyama vya siasa mkoani Shinyanga wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
Mkutano unaendelea
Pamoja na mambo mengine viongozi wa vyama vya siasa walihamasishwa na kuhamasishana kuhubiri amani ya nchi katika kipindi hiki cha uchaguzi ikizingatiwa kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi.
Kushoto ni kamishina wa tume ya taifa ya uchaguzi Asina Omari,kushoto ni mratibu wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga Projestus Rutabanzibwa wakiwa katika mkutano wa tume ya uchaguzi na vyama vya siasa mkoa wa Shinyanga kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
Mkutano unaendelea
Kamishina wa tume ya taifa ya uchaguzi Asina Omari akizungumza wakati wa mkutano wa tume ya uchaguzi na vyama vya siasa mkoa wa Shinyanga kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambapo
alisema katika kipindi hiki cha uchaguzi ni vyema watanzania wakadumisha amani ya nchi kwa kuepuka vitendo vyote vinavyoashiria uvunjivu wa amani ikiwemo wanasiasa kuhamasisha wananchi kulinda kura zao kwenye vituo vya kupigia kura.
Kamishina wa tume ya taifa ya uchaguzi Asina Omari pia alisema kituo cha kupigia kura siyo mahali pa kutangazia matokeo bali ni mahali ambapo zoezi la upigaji kura linafanyika pamoja na kubandika matokeo na kwamba matokeo yote yatatangazwa katika ofisi za kata kwa ngazi ya udiwani,ubunge ngazi ya jimbo na urais yatatangazwa na mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi.
Kaimu mkuu wa tume ya uchaguzi kanda ya kati inayojumuisha mikoa ya Dodoma,Singida,Kigoma,Shinyanga na Tabora Martina Magaulla aliwataka viongozi wa vyama vya siasa kuondoa hofu ya kwamba wataibiwa kura kutokana na kwamba kila chama cha siasa kitakuwa na mawakala wake hivyo kuwaasa kuweka mawakala waaminifu na waadilifu .
Hata hivyo Martina Magaulla alivitaka vyama vya siasa kuweka makawala waaminifu na wazalendo kwa vyama vyao ili kuepuka kununuliwa.
Mratibu wa uchaguzi mkoa wa Shinyanga Projestus Rutabanzibwa akiwa na kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha
Mkutano unaendelea
Mwenyekiti wa chama cha APPT Maendeleo mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Elisiana Tambwe George akifuatilia kwa umakini kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Mkutano unaendelea
Mwandishi wa habari Star Tv Kisali Simba akiwa ukumbini
Mwenyekiti wa chama cha APPT Maendeleo mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Elisiana Tambwe George akichangia mada kwenye mkutano huo
Mwenyekiti wa chama cha CHAUSTA mkoa wa Shinyanga Heri Hussein akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwashauri wanasiasa nchini
kuwa na imani na mawakala wao ili kuufanya uchaguzi ufanyike kwa amani na utulivu kwani hata kukaa nje ya mita 200 haisaidii kitu kwani hakuna kura itakayokuwa inalindwa tofauti na wakala.
Kamishina wa tume ya taifa ya uchaguzi Asina Omari akiwa ukimbini
Mwenyekiti wa chama cha CHAUSTA mkoa wa Shinyanga Heri Hussein akifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
Ninafuatilia kinachojiri hapa.....
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini....
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Social Plugin