Ajali Morogoro!! BASI LA PRINCESS MURO LAGONGANA NA GARI NDOGO,WATU 6 WAFARIKI DUNIA...


Watu sita wamefariki dunia baada ya gari ndogo waliokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na basi la abiria mali ya kampuni ya Princess Muro, lililokuwa likitokea Dar es salaam kuelekea Tunduma, katika eneo la hifadhi ya taifa ya Mikumi, barabara kuu ya Morogoro-Iringa.



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Leonard Paulo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo katika eneo la hifadhi ya taifa ya Mikumi, ikihusisha gari ndogo la abiria aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T 359 BBA iliyokuwa imebeba abiria sita wakiwemo wanawake wawili na wanaume wanne ambayo ilipasuka tairi ya Mbele ya kuyumba ovyo barabarani na kugongana na basi hilo la Princess Muro lenye namba T 160 BBC na kusababisha vifo kwa abiria wote wa Noah.


Amesema basi hilo la abiria aina ya Zangton lililoharibika zaidi mbele huku Noah ikiharibika kabisa, likuwa likiendeshwa na Silos Wilfred (55) mkazi wa Mbeya ambaye anahojiwa na polisi kuhusiana na tukio hilo, na kwamba basi alilokuwa akiendesha lilikuwa na abiria 59 ambao hawakupata madhara makubwa, isipokuwa michubuko kidogo kwa baadhi yao na walitafutiwa usafiri kuendelea na safari.


Katika upekuzi wa miili ya abiria waliokuwa kwenye Noah inayodaiwa kuhusika na ubebaji wa magazeti, viligundulika vitambulisho vimne vya Ali Nduti Mohamed (27), mkazi wa Mbeya,Sani Elion Mkwabe (24) mkazi wa Kunduchi, Patrick Mkelegene (43) mkazi wa Buguruni Malapa na Selemani Omary (30) ambaye makazi yake hàyajaweza kujulikana Mara moja.


Miili ya watu hao waliopoteza maisha imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.
 
Chanzo-Mpekuzi blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527