NEC YATOA MAFUNZO KWA WARATIBU,WASIMAMIZI WA UCHAGUZI NA MAAFISA UCHAGUZI MIKOA YA SHINYANGA NA SIMIYU,ANGALIA PICHA




Hapa ni katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambako leo Kumefanyika mafunzo kwa kwa waratibu wa uchaguzi wa mikoa, wasimamizi wa uchaguzi, maafisa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo katika mikoa ya Shinyanga na Simiyu.Mafunzo hayo ya siku mbili yamelenga kuwafundisha na kubadilishana uzoefu juu ya wajibu na taratibu za mchakato mzima wa uchaguzi kuanzia ,ambapo tutaanza na hatua ya upigaji kura,kuhesabu,kujumlisha kura na kutangaza matokeo ya uchaguzi.Mafunzo hayo yameandaliwa na Tume ya Uchaguzi Tanzania(NEC).Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog Shinyanga



Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga aliyekuwa mgeni rasmi akizungumza katika mafunzo hayo ambapo pamoja na mambo mengine alitumia fursa hiyo kuwataka maafisa wa uchaguzi kusoma kwa makini sheria na kanuni za uchaguzi, hatua itakayosaidia kuwapa uelewa mpana jambo itakayosaidia kufanya kazi yao kwa ufanisi mkubwa.


Rufunga aliwataka wasimamizi hao kuhakikisha vifaa na fomu mbalimbali baada ya kuvipokea kutoka NEC wanavikagua ili kuona kama kuna mapungufu , jambo ambalo litaepusha changamoto ambazo zinaweza kujitokeza ukiwemo ukosefu wa karatasi au majina kukosewa na kubadilishwa vituo.




Mkuu huyo wa mkoa pia alivitaka vyama vya siasa kuweka mawakala wao kwenye kila kituo cha kupigia kura ili kuondoa malalamiko, ambapo aliwatahadharisha kutoingilia kazi za maafisa wa uchaguzi pia maafisa kuwa wa wazi ili kuepuka migongano isiyokuwa ya lazima.



Washiriki wa mafunzo hayo kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini



Washiriki w semina hiyo walisisitizwa juu ya umuhimu wa kusoma vitabu vya maelezo,kanuni,sheria na maadili ya uchaguzi ili kupata uelewa zaidi



Aliyesimama ni msimamizi wa uchaguzi jimbo la Shinyanga mjini,ambaye ni mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Kalinjuna Lewis akizungumza katika semina hiyo ambapo aliwataka wakazi wa manispaa hiyo kuondoa hofu kuwa zinaweza kutokea vurugu kama chaguzi zilizopita na kuwaomba kusahau yaliyopita na kwamba uchaguzi utakuwa wa amani sanjari na matokeo kutangazwa kwa wakati baada ya kukamilika.



Mafunzo yanaendelea



Mafunzo yanaendelea



Tunafuatilia kinachoendelea ukumbini



Mafunzo yanaendelea



Washiriki wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini

Semina inaendelea






Waandishi wa habari wakiwa ukumbini








Afisa uchaguzi kanda ya ziwa kutoka NEC Deogratius Nsanzugwanko, akizungumza na Malunde1 blog nje ya ukumbi ambapoa alisema NEC inakamilisha maandalizi yake ya mwisho ya uchaguzi kwa kuendelea kutoa elimu kwa maafisa watakao husika na zoezi hilo, kuhakikisha changamoto zilizojitokeza chaguzi zilizopita hazijirudii tena huku akiwasisitiza waratibu wa uchaguzi wa mikoa, wasimamizi wa uchaguzi, maafisa uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kuzingatia maelekezo ya elimu waliyopata.


Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog Shinyanga


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527