Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAGOMBEA URAIS TANZANIA WARUDISHA FOMU TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI



Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Ukawa, Mhe. Edward Lowassa akifuatana na Mgombea Mwenza Juma Haji Duni leo wakikamilisha zoezi la kurudisha fomu katika tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Hadi sasa wagombea urais kupitia vyama vya CHADEMA, CCM, TLP, ADC, CHAUMA, UPDP wamerejesha fomu zao katika ofisi za Tume ya uchaguzi na wamekidhi viwango vyote vilivyotakiwa na Tume ya uchaguzi na vimeruhusiwa kuanza rasmi kampeni kuanzia siku ya kesho.

Chama cha ACT Wazalendo nao tayari wamefika ofisi za NEC na kinasubiri muda wa kuingia ndani na kuangaliwa kama kimetimiza viwango vinavyotakiwa na Tume ya uchaguzi.

Angalia ratiba hapa chini

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com