WENYEVITI WA CCM WAMGEUKA LOWASSA,WATANGAZA RASMI KUTOMUUNGA MKONO

Wenyeviti wa chama cha CCM Zanzibar ambao walikuwa wanamuunga mkono Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa katika kuwania urais kwa tiketi ya CCM wametangaza rasmi kutomuunga mkono tena, baada ya kujiengua katika chama hicho na kujiunga na Chadema.

Wakiongea leo Mjini Zanzibar katika mkutano ulioitishwa kutoa tamko la CCM Zanzibar, Mwenyekiti CCM Mkoa wa Mjini, Borafya Silima Juma amesema kuwa awali walikuwa wanamuunga mkono Mhe. Lowassa lakini kwa sasa wamenawa mikono na kuachana nae.


Naye Mjumbe wa kamati Kuu ya (CCM) Bw. Shamsi Vuai Nahodha amekanusha madai kuwa mwenyekiti wa CCM Mh. Jakaya Mrisho Kikwete aliingia na majina yake matano katika vikao vya kuteua mgombea wa urais vilivyofanyika Dodoma.

Bw. Nahodha amesema CCM hakuna utaratibu wa Mwenyekiti kuja na majina yake matano mfukoni katika mikutano ya uteuzi, na kuongeza kuwa utaratibu uliotumika mwaka 2005 ndio utaratibu huo huo uliotumika mwaka 2015, hivyo tuhuma hizo ni za kipuuzi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post