MGOMBEA URAIS EDWARD LOWASSA KUREJESHA FOMU OFISI ZA CHADEMA JUMAMOSI,AGOSTI 01,2015
Taarifa inatolewa kwa vyombo vya habari, wanachama, wafuasi, wapenzi, mashabiki wa CHADEMA na umma wa Watanzania kwa ujumla kuwa baada ya hatua ya kuchukua fomu ya kuwania uteuzi wa ndani ya chama kugombea nafasi ya urais, Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa kesho Agosti 1, 2015 atarejesha fomu yake kwa ajili ya taratibu zingine za ndani ya chama.

Shughuli hiyo itafanyika kuanzia saa 9.00 jioni, ambapo mgombea atakabidhi fomu yake Ofisi ya Katibu Mkuu, Makao Makuu ya Chama, Kinondoni, jijini Dar es Salaam katika hadhara ikayohudhuriwa na viongozi wa chama, wanachama, wafuasi, wapenzi na mashabiki wa CHADEMA kutoka sehemu mbalimbali.


Mheshimiwa Lowassa atarejesha fomu hiyo akiwa mgombea pekee baada ya kuwa ametimiza taratibu za kikatiba hususan kupata wadhamini kutoka mikoa mbalimbali nchi nzima.

Hatua hiyo ya kurejesha fomu itafuatiwa na taratibu zingine za kikatiba, ikiwa ni pamoja na vikao vya uteuzi ambavyo vitaketi kwa mujibu wa ratiba ambayo imeshapangwa na chama.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post