WEKA PEMBENI YA MBUNGE KANGI LUGOLA KUVAA KININJA BUNGENI,HUYU MBUNGE KAINGIA NA CHUPI KABISA




Unamkumbuka yule Mbunge wa Mwibara Kangi Lugola aliyeingia Bungeni na bidhaa za kichina huku akiilaumu Serikali kushindwa kutumia rasilimali zake na kutegemea bidhaa za nje?.

Hii nyingine imetokea Zimbabwe na kuzua kizaazaa baada ya Mbunge wa upinzaniPriscilla Misihairabwi kutinga Bungeni akiwa na nguo za ndani za wanawake huku akisisitiza hatma ya raia wake maskini kutokuwa na uwezo wa kununua nguo hizo.

Katika kikao chicho cha bunge kilichokuwa kikirushwa live na Televisheni ya Taifa, mbunge huyo wa Chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change ‘MDC‘ alitoa mfuko wa plastiki uliokuwa na nguo hizo.


Bunge la Zimbabwe

Baada ya kutoa akamuuliza Waziri wa Fedha na sera za serikali kuhusiana na uingizwaji wa nguo hizo za mtumba ambazo bei yake ni ndogo na husababisha madhara kwa akina mama.

Akijibu swali hilo Waziri wa Fedha Patrick Chinamasa alimtania Mbunge huyo kutokana na uamuzi wake wa kubeba nguo za ndani za akina mama lakini akasema Wizara yake inachunguza suala hilo.

Kufuatia kitendo hicho Mbuge huyo alitolewa ndani ya ukumbi wa Bunge na wabunge wa chama tawala cha ZANU PF kwa madai ya kutumia matamshi ya kibaguzi.

Uchumi wa Zimbabwe umedorora miaka ya hivi karibuni hali iliyosababisha viwango vya umaskini kuongezeka kutokana na kuwepo idadi kubwa ya watu wasio na ajira.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527