Maskini!! KUMBE HUYU DADA NDIYO ALIZIKWA NA GODORO,KITANDA,SIMU,DAFTARI LA MICHANGO,FEDHA,KITANDA NA VITU VINGINE KIBAO...HUKO SIMIYU



Marehemu, Jesca Onesmo enzi za uhai wake.

Wanachi wakitaharuki vyombo vilivyoweka juu ya kaburi marehemu, Jesca Onesmo.


Wahenga walisema ukisitajabu ya Musa utaona ya Firauni, hivi ndivyo ilivyokuwa kwa wananchi wa mji wa Bariadi mkoani Simiyu waliofurika katika kaburi la marehemu, Jesca Onesmo (28), ambaye alifariki kisha kuwekewa samani na vyombo vyake mbalimbali juu ya kaburi lake.


Ilikuwa asubuhi ya saa mbili, Julai 7, mwaka huu ambapo baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Marambo, Bariadi waliokuwa wamepata msiba walipokwenda eneo la Makaburi ya Kidinda kwa ajili ya kutafuta mahali pa kuchimba kaburi, walipofika eneo hilo walipigwa na butwaa baada ya kuona kaburi moja likiwa limewekewa vitu juu, hali ambayo ilitafsiriwa kuwa amezikwa navyo.


Mwandishi wetu baada ya kupewa habari hiyo alifika katika eneo hilo na kukuta samani za ndani, godoro na vyombo mbalimbali vikiwa vimerundikwa juu ya kaburi hilo na baada ya uchunguzi ikajulikana kuwa ni kaburi la Jesca.


Mwananchi mmoja ambaye aliomba jina lake lisitajwe alisema: “Kwa kweli hili ( la kurundikwa vyombo vyake juu ya kaburi) limetushangaza sana na ni la kwanza kutokea hapa Bariadi, hata sisi hatujui sababu lakini labda ni ushirikina.”


Baada ya tukio hilo polisi waliarifiwa ambapo walifika makaburini na kuamua kuvipakia vyombo hivyo kwenye gari la polisi na kuvipeleka kituoni na baada ya kufika huko walivifanyia upekuzi na kugundua vitu mbalimbali.


Habari za kipolisi zinasema walikuta pochi ya marehemu ambayo ndani yake ilikuwa na shilingi 13,000 pamoja na simu ndogo lakini pia walifanikiwa kukuta cheti cha hospitali kilichoonesha marehemu alikuwa mgonjwa na alikuwa anatumia dawa kila siku.


Aidha, walipata pia daftari la mchango wa kifo ambalo lilionesha kuwa alichangiwa na walipata jina na namba za simu ya dada yake (jina linahifadhiwa) ambaye inadaiwa kuwa ndiye aliyehusika kumzika ingawa baada ya kumpigia simu hakupokea na walipomfuatilia walikuta ametoroka na familia yake, hadi sasa haijafahamika alipo.


Hata hivyo, baada ya tukio hilo kutangazwa na vyombo vya habari baadhi ya wananchi walidai kuwa marehemu alikuwa anaishi na mume wake huko wilayani Kahama na hawakujua nini kilitokea hadi kuzikwa na kurundikiwa vyombo juu ya kaburi lake.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, ACP Gemini Mushy amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo.


“Tukio hilo lipo lakini tunaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo chake na sababu ya kumzika na vyombo vyake,” alisema kamanda huyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post