Haya Sasa!! MTANGAZAJI MAARUFU WA RADIO FREE AFRICA ATANGAZA RASMI KUWANIA UBUNGE KATIKA JIMBO JIPYA LA USHETU HUKO KAHAMA

Mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa William Bundala maarufu kwa jina la “kijukuu cha bibi k” akiwa amebebwa juu na wakazi wa Ushetu wakati wa mkutano wake wa kutangaza nia kuwania ubunge katika jimbo jipya la Ushetu wilayani Kahama


Mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa William Bundala maarufu kwa jina la “kijukuu cha bibi k” akiwa amebebwa juu na wakazi wa Ushetu wakati wa mkutano wake wa kutangaza nia kuwania ubunge katika jimbo jipya la Ushetu wilayani Kahama



Mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa William Bundala maarufu kwa jina la “kijukuu cha bibi k” akitangaza nia kuwania ubunge katika jimbo jipya la Ushetu wilayani Kahama



Mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa William Bundala maarufu kwa jina la “kijukuu cha bibi k” akizungumza na wakazi wa Ushetu wakati wa mkutano wake wa kutangaza nia kuwania ubunge katika jimbo jipya la Ushetu wilayani Kahama



Mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa William Bundala maarufu kwa jina la “kijukuu cha bibi k” katika pozi



Mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa William Bundala maarufu kwa jina la “kijukuu cha bibi k” akiwajibika katika kazi yake ya uandishi wa habari



Mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa William Bundala maarufu kwa jina la “kijukuu cha bibi k” akiwa katika moja ya mikutano muhimu
********
Siku moja tu baada ya Tume ya Uchaguzi nchini Tanzania kutangaza majimbo mapya ya Uchaguzi,Mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa William Bundala maarufu kwa jina la “Kijukuu cha Bibi K” ametangaza rasmi kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania Ubunge katika Jimbo la jipya la Ushetu katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu mkoani Shinyanga,kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.

Bundala ametangaza kuingia kwenye mchakato wa kugombea kuteuliwa na Chama ili aweze kupeperusha bendara ya Chadema/UKAWA katika uchaguzi mkuu ujao katika mkutano wake wa kutangaza nia uliofanyika katika Kijiji cha Bogomba “B” kata ya Ubagwe wilayani Kahama.

Mtia nia huyo alisema endapo Chama chake kitampitisha na hatimaye kushinda Ubunge katika Jimbo hilo atahakikisha anasukuma kasi ya maendeleo katika jimbo hilo jipya lenye Rasimali nyingi kupitia nafasi yake na wajibu kama anavyotakiwa Mbunge Kufanya.

Alisema kuwa dhamira yake imemsuta kwenda kuwatumikia wananchi wa wilaya hiyo ambayo yeye ni mzawa na kuwa atahakikisha anapigania maendeleo ya wananchi kwa kasi huku akiondoa uonevu kwa waandishi wa habari na watumishi wengine serikalini na katika halmashauri za
wilaya.

Sambamba na hayo amesema kuwa sababu nyingine iliyomsukuma ni kuona wagombea wengine wanaolitaka jimbo hilo hawako kwa ajili ya ukombozi wa jimbo hilo bali wako kwa ajili ya maslahi binafsi kutokana na asilimia kubwa ya wagombea hao si wakazi wa eneo hilo na kwamba hawafahamu matatizo ya wana ushetu kama anavyoyafahamu yeye.

Aliongeza kuwa akifanikiwa kuukwaa Ubunge pia atasimamia kuhakikisha Jimbo hilo jipya linapata Chuo cha ufundi kwa ajili ya vijana wanaomaliza darasa la saba na kidato cha nne kupata elimu jambo lilatalopunguza wimbi la ukosefu wa ajira kwa vijana.

Bundala alisema kipaumbele kingine atakachoshughulikia ni pamoja na kusimamia na kutoa elimu ya Sheria kupitia wanasheria ambao watazunguka katika kata kutoa elimu hiyo hususan katika maswala ya umiliki wa Ardhi,Mirathi,haki za wakulima na wafugaji pamoja na haki za raia na mali zao kwa ujumla.

Akizungumzia kuhusu suala la michezo katika jimbo hilo, Bundala alisema kuwa kupitia Kijukuu Cup atahakikisha anashirikiana na halmashauri na wadau wa michezo kuhakikisha halmashauri ya ushetu inapata timu ya kucheza ligi kuu Tanzania Bara.

Awali Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CHADEMA (BAVICHA) Halmashauri ya Ushetu Emmanuel Magema aliwataka vijana wote kuungana ili kumuunga mkono kijana mwenzao aliyejitokeza na kuonesha nia ya kutaka kuongoza akiwa Mbunge wa jimbo hilo.

Wilaya ya Kahama kwa sasa ina halmashauri za wilaya tatu za
Msalala,halmashauri ya mji wa Kahama na halmashauri mpya ya Ushetu na kufanya majimbo ya uchaguzi kuwa matatu.


Katika kinyang’anyiro cha Ubunge katika jimbo jipya la Ushetu kuna watu zaidi ya watano wanaotajwa kulimendea jimbo huku wagombea wa CHADEMA wakionekana kuungwa mkono na makundi mengi hususan vijana.

Na Mwandishi Maalum wa Malunde1 blog Ushetu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post