MAGUFULI AFUNIKA DAR_ SHUHUDIA HAPA MAELFU YA WATU WALIOJITOKEZA KUMPOKEA,NI BALAA TUPU

Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe akihutubia wakazi wa jiji la Dar es Salaam.Mgombea  huyo wa urais kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akiambatana na mgombea mwenza Bi Samia Suluhu Hassaan wamepokelewa na maelfu ya wakazi wa jiji la Dar-es-Salaam na viunga vyake huku mgombea Dkt Magufuli akisema anakerwa na watendaji wa serikali wasiotimiza wajibu wao.

Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe akihutubia wakazi wa jiji la Dar es Salaam.Mgombea huyo aliwasili katika uwanja wa Mbagala Zakiemu manisipaa ya Temeke jijini Dar-es-Salaam na akiwa katika gari la wazi na kuwasalimia wananchi waliofurika kushuhudia mapokezi hayo, ambapo viongozi mbalimbali wa chama na serikali wa manisipaa zote za jiji la Dar-es-Salaama bila kujali itikadi zao walimshangilioa kwa furaha na bashasha kubwa.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar Es Salaam akimpokea Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam tayari kwa kujitambulisha kwa wakazi wa jiji hilo.

Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakati wa mapokezi kwenye uwanja wa ndege wa Dar es salaam.

Wakazi wa Mbagala wakiwa wamejipanga barabarani kumuona mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli .

Katibu wa Itikadi na uenezi Nape Nnauye akiwasili kwenye viwanja vya Zakheem Mbagala akiwa kwenye usafiri wa Boda boda.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimu wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza mgombea wa nafasi ya Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli.

Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa mkutano wa Mbagala Zakheem tayari kwa kujitambulisha kwa wakazi wa Dar es Salaam.


Dk. John Pombe Magufuli mgombea wa Urais kupitia CCM akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Kinondoni Mheshimiwa Idd Azzan wakati akiwasili kwenye uwanja wa mikutano Zakheem Mbagala.


Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Ramadhan Madabida akiwasalimu wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwenye mkutano wa kumtambulisha mgombea wa Urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli kwa wakazi wa Dar es Salaam.Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akiwatambulisha viongozi mbali mbali waliomsindikiza mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli kwenye viwanja vya mikutano vya Mbagala Zakheem.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa jiji la Dar es Salaam kabla ya kumkaribisha mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kujitambulisha na kuwasalimia wakazi wa Dar es Salaam.

Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Dar es Salaam kwenye viwanja vya Zakheem Mbagala kwenye mkutano wake wa kujitambulisha kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam ambapo aliahidi kuwatumikia wananchi na kutenda haki.Mgombea Mwenza wa CCM Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Mbunge wa Temeke Mhe. Abbas Mtemvu kwenye mkutano wa hadhara wa kumtambulisha mgombea wa CCM kwa nafasi ya Urais Mhe. John Pombe Magufuli

Ndugu, Jamaa na wafanyakazi wenzake Dk. John Pombe Magufuli wakisikiliza kwa makini hotuba kwenye mkutano huo.

Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akipiga ngoma za tumba pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye kwenye jukwaa la bendi ya TOT mara baada ya kumaliza kujitambulisha na kuhutubia wakazi wa jiji la Dar es Salaam

Waandishi wa habari wakiwa kazini kwenye mkutano wa Dk. John Pombe Magufuli jijini Dar es salaam.Akiwasalimia wananchi hao mgombea huyo Dkt John Pombe Joseph Magufuli amewaambia wananchi hao waendelee kumuombea na kuwa atafanya kazi waliyomtuma na kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi wa kishindo, na kusisitiza kuwa yeye ni mpole ila anachukia watendaji wa serikali wazembe wasiotimiza wajibu wao na kuwaacha Wananchi wakiwa na kero mbalimbali bila kuzipatia ufumbuzi. Picha zote kwa hisani ya CCM Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post