ANGALIA PICHA-MAZISHI YA NGULI WA MUZIKI WA DANSI BONGO BANZA STONE,LEO MAKABURI YA SINZA JIJINI DAR ES SALAAM

Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lililobeba mwili wa marehemu Banza StoneMke wa Rais Mama Salma Kikwete akilakiwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrer Mngereza alipowasili kujiunga na familia na waombolezaji katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015. 

Marehemu Banza Stone, aliyefariki jana mchana baada ya kuugua kwa muda mrefu, amezikwa jioni hii katika makaburi ya Sinza. Marehemu Banza Stone atakumbukwa kwa umahiri wake wa utunzi na uimbaji alipokuwa na bendi mbalimbali zikiwemo Twanga Pepeta, Tot na Extra Bongo.


Jeneza lenye mwili wa marehemu Ramadhani Masanja "Banza Stone" likitolewa nyumbani tayari kwa mazishi Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.

Waombolezaji

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Ubungo Mhe. John Mnyika alipowasili kujiunga na familia na waombolezaji katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitambulishwa kwa Katibu wa bendi ya TOT, Gasper Tumaini, ambako marehemu Banza Stone aliwahi kufanya kazi enzi za uhai wake

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpa pole kaka wa marehemu alipowasili kujiunga na familia na waombolezaji katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa pole kwa wana familia na waombolezaji katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimfariji mama mzazi wa marehemu katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na kiongozi wa bendi ya African Stars Twanga Pepeta Asha Baraka katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimfariji Haji Ramadhani Masanja, mtoto wa marehemu katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na Haji Ramadhani Masanja, mtoto wa marehemu katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.

Jeneza lenye mwili wa marehemu Ramadhani Masanja "Banza Stone" likitolewa nyumbani tayari kwa mazishi Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.

Waombolezaji wakilia kwa uchungu wakati mwili wa Banza Stone ukipelekwa mazikoni

Mama Salma Kikwete, Asha Barka na mama wa marehemu wakiwa na nyuso za huzuni wakati mwili wa merehemu Banza Stone ukipelekwa mazikoni

Mama Salma Kikwete akiagana na kiongozi na mwimbaji wa African Stars wana Twanga Pepeta ambaye alifanya kazi kwa karibu na Banza Stone tokea kuanza kwa bendi hiyo

Mama Salma Kikwete akiaga waombolezaji katika msiba wa mwanamuziki Ramadhani Masanja "Banza Stone" Sinza Lion jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 18, 2015.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post