ZIKO HAPA PICHA 65- RAIS KIKWETE AONGOZA MAELFU YA WATU MAZISHI YA MUFTI ISSA SHAABAN SIMBA MAKABURI YA NGUZO NANE SHINYANGA,LOWASSA,MEMBE,NYALANDU,NGELEJA,SUMAYE WALIKUWEPO


Mufti Issa Shaaban bin Simba enzi za uhai wake


Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ameongoza maelfu ya waumini wa dini ya kiislamu na watu mbalimbali wenye mapenzi mema kumzika Shehe mkuu wa Tanzania Mufti Issa Shaban Simba katika makaburi ya waislam ya Nguzo nane mjini Shinyanga.

Mazishi hayo yamefanyika leo jioni na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini ya kiislamu,wakristo na viongozi wa serikali ,wanasiasa ambao walijitokeza kumzika Mufti Simba aliyefariki dunia jana akipatiwa matibabu kutokana na kusumbuliwa sana na sukari,Shinikizo la Damu (BP)  pamoja na Figo.

Katika mazishi hayo,mawaziri wakuu wastaafu Mheshimiwa Edward Lowassa na Fredrick Sumaye walikuwepo,viongozi wengine ni mheshimiwa Lazaro Nyalandu,Benard Membe,William Ngeleja,Patrobas Katambi,Stephen Masele,askofu Liberatus Sangu n.k

Mwili wa marehemu uliwasili mchana mjini Shinyanga ukitokea jijini Dar es salaam na kufikishwa nyumbani kwa marehemu katika mtaa wa Majengo kata ya Kambarage katika manispaa ya Shinyanga.


Baadaye mwili ulipelekwa katika msikiti wa  Masjidu Thaqafal Abdallah Islamiya uliopo Majengo mjini Shinyanga kwa ajili ya sala ya alasiri/kuombewa dua kisha mwili huo kupelekwa katika makaburi ya waislamu ya Nguzo Nane kwa ajili ya Mazishi.

Mufti Simba alizaliwa mwaka 1939,ameacha mjane na watoto 11.  
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,ndugu Kadama Malunde alikuwepo eneo la tukio ametuletea picha zaidi ya 60 angalia hapa chini

Nyumbani kwa marehemu- MTAA WA MAJENGO MJINI SHINYANGA-Ndugu wa marehemu wakijiandaa kupkea mwili wa marehemu ukitoka jijini Dar es saalam
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj  Mussa Salum akiongea jambo na meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam nyumbani kwa marehemu mtaa wa Majengo mjini Shiyanga
Shehe  wa wilaya ya Shinyanga akitoa maelekezo msibani
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu

Viongozi mbalimbali wa dini ya kiislam nchini wakiwa msibani

Waombolezaji wakiwa msibani

Waombolezaji wakiwa msibani

Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj  Mussa Salum akiongea jambo na waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa nyumbani kwa marehemu

Mbunge wa jimbo la Solwa Ahmed Salum akiwa na mheshimiwa Lowassa

Mawaziri wastaafu Edward Lowassa na Fredrick Sumaye wakisalimiana msibani

Maelfu ya waombolezaji wakiwa msibani
Jeneza lililobeba mwili wa Mufti Alhaj Sheikh Shaaban bin Simba kuelekea katika msikiti wa wa  Masjidu Thaqafal Abdallah Islamiya uliopo Majengo mjini Shinyanga kwa ajili ya sala ya alasiri

Mwili wa marehemu ukiwa kwenye jeneza

Mwili wa marehemu ukipelekwa msikitini

Mwili wa marehemu ukipelekwa msikitini

Waombolezaji wakiwa wamejipanga barabarani

Mbunge wa Kishapu Suleiman Nchambi akitoa maelekezo kwa waombolezaji waliokuwa barabarani
Baadhi ya waombolezaji wakiwa nje ya msikiti
Mwili wa marehemu ukiingizwa msikitini  kwa ajili dua ya kumuombea marehemu.Msikiti huo wa Ijumaa wa Majengo mjini Shinyanga ni ule ambao kabla Mufti Issa Bin Shaban Simba alikuwa shehe wa msikiti huo
Akina mama hawakuwa nyuma,wakaamua kujipanga barabarani

Waombolezaji wakiwa barabarani kusubiri mwili wa marehemu utolewe msikitini na kuupeleka makaburini

Sheikh wa mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya(kulia) akiwa katika makaburi ya Nguzo nane mjini Shinyanga

Waombolezaji wakiwa katika makaburi ya Nguzo nane mjini Shinyanga

Wakazi wa Shinyanga wakiwemo wakuu wa wilaya za Kahama na Kishapu wakiwa katika makaburi ya Nguzo nane

Viongozi mbalimbali wakiwa katika makaburi ya Nguzo nane

Viongozi mbalimbali wakiwa makaburini

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja(kulia) akiwa nje ya geti la makaburi ya Nguzo nane
Waombolezaji wakigombania kuingia makaburini

Rais Kikwete akiwa katika makaburi ya Nguzo nane,wa kwanza kushoto ni kadhi mkuu wa Tanzania Sheikh Mnyasi,akifuatiwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga
Waombolezaji wakiwa katika makaburi ya Nguzo nane
Shughuli za Mazishi zinaendelea
Waombolezaji wakiwa makaburini
Rais Kikwete akiwa ameshika tama makaburini

Mdogo wake na marehemu Ramadhani Simba akiweka udongo kaburini

Rais Kikwete akiweka udongo kaburini

Kadhi mkuu wa Tanzania Sheikh Yusuph Bin Abdallah Mnyasi akiweka udongo kaburini

Mheshimiwa Fredrick Sumaye akiweka udongo kaburini

Mheshimiwa Edward Lowassa akiweka udongo kaburini
Mheshimiwa Khamis Mgeja akiweka udongo kaburini
Mheshimiwa Bernard Membe akiweka udongo kaburini

Rais Kikwete akiwa katika makaburi ya Nguzo nane

Mazishi yanaendelea

Waombolezaji wakiwa eneo la tukio
Kaburi la Mufti Alhaj Sheikh Shaaban bin Simba katika makaburi ya Nguzo nane mjini Shinyanga.

Dua inaendelea

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akimpokea mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete nyumbani kwa marehemu katika mtaa wa Majengo mjini Shinyanga kwa ajili ya kuwapa mkono wa pole ndugu na jamaa wa marehemu

Rais Kikwete akishikana mkono na sheikh wa mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya

Rais Kikwete akishikana mkono ana askofu wa kanisa katoliki Jimbo la Shinyanga Liberatus Sangu

Rais Kikwete akiwa nyumbani kwa marehemu

Rais Kiwete akiwapungia mkono waombolezaji akiondoka mjini Shinyanga

Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu
Mheshimiwa William Ngeleja akiwa nyumbani kwa marehemu
Mhehimiwa William Ngeleja akiendelea kutoa mkono wa pole
Mheshimiwa Ngeleja akiwa nyumbani kwa marehemu Mufti Simba
Mheshimiwa Ngeleja akimpa mkono wa pole shemeji yake na marehemu bwana Mbaruku Yusuph
Mheshimiwa Ngeleja akiwa nyumbani kwa marehemu mufti Simba
Mheshimiwa Ngeleja akiwa nyumbani kwa marehemu

Mheshimiwa Lazaro Nyalandu akizungumza nyumbani kwa marehemu baada ya mazishi
Mheshimiwa Lazaro Nyalandu akizungumza nyumbani kwa marehemu baada ya mazishi,nyuma yake ni mwenyekiti wa baraza la vijana Chadema taifa,Patrobas Katambi.

 Mheshimiwa William Ngeleja akiwa nyumbani kwa marehemu akitoa mkono wa pole kwa ndugu jamaa na marafiki


 Mheshimiwa Ngeleja akitoa mkono wa pole kwa mtu mmoja baada ya mwingine

 Mheshimiwa Ngeleja akiwa msibani

 Mheshimiwa Ngeleja akiondoka msibani.

 Marehemu alijiunga na BAKWATA mwaka 1968 na amekuwa mwalimu wa chuo katika mikoa mbalimbali ya Mwanza, Bukoba na Mwaka 1970 alikuwa Shekhe wa Mkoa wa Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post