RAIS KIKWETE AMLILIA MUFTI ALHAJ SHEIKH SHABAAN BIN SIMBA ,MAZISHI YATAFANYIKA LEO JIONI SHINYANGA

 Sehemu ya wanawake waliofika nyumbani kwa Marehemu  Mufti Alhaj Sheikh Shabaan Issa Bin Simba Mikocheni B jijini Dar es Salaam .


MWILI wa  Mufti ,Alhaj Sheikh Shaban Issa Bin Simba unatarajia kusafirishwa leo Jumanne Juni 16 saa 3 asubuhi, kuelekea mkoani Shinyanga kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Mufti ,Alhaj Sheikh Shaban Issa Bin Simba enzi za uhai wake

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata), Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj  Mussa Salum, amesema mwili wa marehemu utaswaliwa kesho (leo) katika Msikiti wa Msilimu, viongozi mbalimbali wa dini na serikali watakuwepo.

Amesema marehemu amefikwa na umauti huo, baada ya kusumbuliwa sana na sukari,Shinikizo la Damu (BP)  pamoja na Figo.

Hata hivyo amesema kuwa juzi (Jumapili) Mufti alifanyiwa oparesheni ya figo katika Hospitali ya TMJ Jijini Dar es Salaam.

Salum amesema marehemu anatarajiwa kuzikwa leo Jumanne majira ya saa kumi alasiri mkoani mkoani Shinyanga .

Sheikh Mkoa wa Dar es Salaam,Alhaj Sheikh Alhad Mussa Salum akibadilishana mawazo na Sheikh wa Mkoa wa Kigoma Hassan Kiburwa walipofika nyumbani kwa Marehemu Mufti ,Mikocheni B  jijini Dar es Salaam
Kulia ni Sheikh wa Mkowa Dar es Salaam,Alhaj Sheikh Alhad Mussa Salum akiwa na baadhi ya Masheikh waliofika Nyumbani kwa Marehen Mufti,Shabaan Issa Bin Simba Mikocheni B Jijini Dar es Salaam.
 @@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametuma
salamu za rambirambi kwa Waislamu wote nchini na Baraza Kuu la Waislamu
Tanzania  (BAKWATA)) kufuatia kifo cha Sheikh Mkuu wa Tanzania  Mufti
Sheikh  Issa Bin Shaaban Simba.

Marehemu Mufti amefariki  tarehe 15/6/2015 asubuhi katika hospitali ya TMJ – DSM alipokuwa amelazwa akisumbuliwa
na ugonjwa wa sukari na shinikizo la damu (pressure).

"Kifo kinaleta huzuni,hata hivyo Kifo hakizuiliki, hatuna budi kukikubali na ni wajibu wetu kumuombea
Sheikh Mkuu kwa Mola wetu ampe mapumziko ya milele".


 Rais Kikwete ametuma salamu hizo za rambirambi kupitia kwa
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum.

"Nawaombea subra wana familia, ndugu, jamaa, waislamu wote
na wana jamii kwani Mufti alikua kiongozi katika Jamii yetu'
Rais amesema na kueleza kuwa "Kamwe

mchango wake hautasahaulika katika jamii yote kwa Ujumla na hakika sote tutamkumbuka" ameongeza.

Marehemu alijiunga na BAKWATA mwaka
1968 na amekuwa mwalimu wa chuo katika mikoa mbalimbali ya Mwanza, Bukoba na Mwaka 1970 alikuwa Shekhe wa Mkoa wa Shinyanga.

Rais amemuelezea Marehemu Mufti kama
mwalimu katika jamii ambaye alikua na uzoefu wa hali ya juu na mwenye kupenda dini yake na kuitumia kwa manufaa ya jamii iliyomzunguka

"Amekua mwalimu imara na mtu wa kutumainiwa na kutegemewa katika uislamu na jamii kwa ujumla, hakika
tutamkumbuka siku zote' Rais Kikwete ameongeza.

Shekhe Issa Bin Shaaban Simba alikuwa
na uzoefu  mkubwa ndani ya BAKWATA na  aliwahi kukaimu nafasi ya mufti kwa siku 90, baada ya kifo cha Mufti Hemed mwaka 2002.

Baada ya hapo akasimamia mchakato wa uchaguzi
wa Mufti Mkuu na baadaye 2003 akachaguliwa kuwa Mufti Mkuu wa Tanzania.

Mwenyezi Mungu ailaze roho yake
pahali pema Peponi, Amina.
Imetolewa na :

Premi Kibanga,

Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,

Ikulu-DSM

15 Juni, 2015

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post