WATANGAZA NIA URAIS KUPITIA CCM WAANZA KUCHUKUA FOMU HUKO DODOMA

Zoezi la uchukuaji fomu za kuwanaia urasi wa jamhuri ya mungano wa Tanzania kwa awamu ya tano kupitia Chama Cha Mapinduzi umeanza rasmi mjini Dodoma kwa makada wa chama hicho waliotangaza nia ya nafasi hiyo ya juu ya uongozi wa Tanzania.


Mji wa Dodoma pamoja na viunga vyake umepambwa kwa rangi za kijani na manjano za makada na wafuasi wa chama hicho ambao wamewasindikiza wagombea wanao waunga mkono.

Zoezi hilo limeanza mapema majira ya saa nne asubuhi, saa tano na saa kumi na moja jioni kwa wagombea wa nafasi hiyo, kufika makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma, kuchukua fomu tayari kwa zoezi la kutafuta wadhamini ili kuwaunga mkono kutoka Tanzania bara visiwani.


 
Akiongea waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu hizo, mheshimiwa Steven Masatu Wasira amesema kuwa ana nia ya dhati ya kuwatumikia wanannchi, kwa kusimamia ukuaji wa uchumi, kwa kufufua viwanda na kuboresha kilimo ambacho ni tegemeo kubwa la ajila kwa wananchi na kukomesha rushwa kubwa na ndogo, wakati wa kupata huduma mbalimbali nchini.


 
Waliokwisha chukua fomu tayari ni Mheshimiwa Professa Mark Mwandosya, Mheshimiwa Stiven Masatu Wasira, na balozi Amina Salumu Ally.


Wanaotarajiwa kuchukua fomu siku ya Alhamis ni mhesimiwa John Pombe Magufuri, aliyeoneonekana viwanja hivyo akimalizia hatua za mwisho, Mheshimiw Edward Lowasa, Mh: Frederick Sumaye, Mh:Amosi Robert Siantemi, Mh:Mohamedi Gharib Bilal,na balozi Ally Karume.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post