PICHA na HOTUBA_ MAKONGORO NYERERE AMLIPUA LOWASSA AKICHUKUA WADHAMINI WAKE SHINYANGA,AFIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU MUFTI SIMBA


Mtangaza nia kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao Charles Makongoro Nyerere leo amekamilisha ziara ya  kutafuta wadhamini mikoani.Ziara yake ameikamilisha katika mkoa wa Shinyanga.Katika hotuba yake ya kukamilisha ziara yake,Makongoro Nyerere amekemea vitendo vya mafisadi aliodai hawazidi 20,anaowafahamu sura,majina na tabia zao ambao wamekuwa kikwazo hata kwa rais Jakaya Mrisho Kikwete,aliodai kuwa wengi ni marafiki zake na rais.Mwandishi wetu Kadama Malunde,ametuletea picha na HOTUBA NZITO YA MAKONGORO akizungumzia ufisadi ndani ya CCM huku akimtaja Mheshimiwa Edward Lowassa kuwa hafai kuwa rais wa Tanzania(HOTUBA IKO MWISHONI MWA PICHA HAPA CHINI
Hapa ni katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi za Wilaya ya Shinyanga mjini,mkoa wa Shinyanga.Aliyesimama ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Kanali mstaafu Tajiri Maulid akimkaribisha  mheshimiwa Makongoro Nyerere(ambaye ni mtoto wa baba wa taifa Julius Kambarage Nyerere),aliyefika leo Shinyanga kuchukua fomu ya majina ya wadhamini 30 kama alivyohitaji ili agombee urais katija uchaguzi mkuu 2015.
Mtia nia ya urais Makongoro Nyerere akiwasalimia wadhamini wake kutoka mkoa wa Shinyanga waliojitokeza kumpokea katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga
Makongoro akizungumza wakati wa kuchukua fomu ya majina 30 ya wadhamini kutoka mkoa wa mwisho kati ya mikoa yote aliyozunguka kusaka wadhamini

Makongoro Nyerere wakati wa kuchukua wadhamini wake 30 katika ofisi za wilaya ya Shinyanga mjini mkoani Shinyanga kama alivyohitaji ambapo amesema CCM inapoteza mwelekeo kutokana na baadhi ya wanachama wake kuendekeza ufisadi.


Pichani ni wadhamini wake kutoka Shinyanga-Makongoro Nyerere amewataka wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi kuhakikisha wanatenda haki kupitisha jina la mgombea atakayerudisha heshima ya CCM iliyopotea na kwamba endapo CCM itakosea uteuzi wa kumsimika mgombea makini nchi itakwenda na upinzani.
Makongoro amesema watanzania wanaendelea kuwa maskini kutokana na tabia mbaya ya baadhi ya mafisadi ambao wamekuwa wakimsumbua rais Jakaya Kikwete na kuonekana hafanyi kazi kumbe tatizo ni hao marafiki zake

Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Charles Sangura(kulia) akikabidhi fomu ya majina ya wadhamini wa mtia nia ya urais Makongoro Nyerere

Makongoro Nyerere akipokea fomu yenye majina ya wadhamini 30 kutoka mkoa wa Shinyanga
 
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Charles Sangura akikabidhi fomu ya majina ya wadhamini wa mtia nia ya urais Makongoro Nyerere
Makongoro Nyerere akishikana mkono na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Kanali mstaafu Tajiri Maulid
Makongoro Nyerere akionesha mkoba uliobeba Fomu zake baada ya kukamilisha zoezi la kupata wadhamini na kuelekea Dodoma kwa ajili ya kukabidhi fomu hizo makao makuu na kubiri jina lake lipitishwe na kikao cha halmashauri kuu ya CCM Julai,12 mwaka huu
Charles Makongoro Nyerere amesema baada ya kazi ya kutafuta wadhamini chini ya Chama Cha Mapinduzi bila kuvunja utaratibu na kanuni kwa mikoa mbalimbali kutoka Tanzania bara na visiwani  mwishowe amemaliza kwa wakati na kesho tarehe 19/06/2015 atarudisha fomu pale makao makuu ya chama Dodoma.
Picha ya pamoja,Makongoro Nyerere na wadhamini wake kutoka mkoa wa Shinyanga juu ya jengo la CCM wilaya ya Shinyanga mjini
Makongoro Nyerere na wadhamini wake kutoka mkoa wa Shinyanga juu ya jengo la CCM wilaya ya Shinyanga mjini

HAPA NI NJE NYUMBANI KWA HAYATI MUFTI ISSA SHAABAN SIMBA KATIKA MTAA WA MAJENGO MJINI SHINYANGA.Akiwa mkoani Shinyanga Makongoro amekwenda kumpa mkono wa pole mjane wa aliyekuwa mufti mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Shaaban bin Simba ,Mwanagoso nyumbani kwake katika mtaa wa Majengo mjini Shinyanga na kutoa ubani.Pichani ni Makongoro Nyerere akishikana mkono na Shehe wa wilaya ya Shinyanga Sudy Kategire

Makongoro Nyerere akizungumza jambo na kaka yake na hayati Mufti Simba,Ramadhan Simba alipofika kuwapa mkono wa pole
Makongoro Nyerere akiwa nyumbani kwa hayati Mufti Simba
Makongoro akimpa mkono wa pole mjane wa aliyekuwa mufti mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Shaaban bin Simba ,Mwanagoso nyumbani kwake katika mtaa wa Majengo mjini Shinyanga pamoja na kutoa ubani 
Makongoro Nyerere akiwa ndani ya nyumba ya hayati Mufti Simba
Makongoro Nyerere akimpa mkono wa pole mjukuu wa hayati Mufti Simba

IFUATAYO NI HOTUBA NZITO ALIYOITOA MAKONGORO NYERERE WAKATI AKICHUKUA WADHAMINI WAKE MKOANI SHINYANGA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post