News Alert! ASKARI SABA WA USALAMA BARABARANI WAGONGWA GARI HUKO ARUSHA


Askari saba wa Jeshi la Polisi nchini, kitengo cha Usalama Barabarani, wamenusurika kifo kufuatia ajali iliyohusisha gari la Polisi na gari moja binafsi mjini Arusha leo hii.

Gari zilizohusika katika ajali hiyo, zote ni aina ya Toyota Land Cruiser, moja likiwa ni mali ya Jeshi la Polisi nchini, na jingine lenye namba T 549 ADM, ambalo ni mali ya kampuni moja ya Utalii mkoani humo.

Jeshi la Polisi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo, kupitia taarifa fupi iliyopatikana kwenye mtandao wa kijamii unaoendeshwa na Mabalozi wa Usalama Barabarani, taarifa ya Jeshi hilo imesomeka kama ifuatavyo;

"Ni kweli ajali imetokea na kusababisha majeruhi 7 wakiwa ni askari wa U/barabarani Arusha. Chanzo cha ajali ni mwendokasi wa dereva hatimaye kushindwa kumudu gari na kusababisha gari kuhama lane nyingine na kugonga gari la Polisi lililokuwa linakuja mjini Arusha. Dereva alikuwa amelewa na kwa kiwango kikubwa baada ya kupimwa. Majeruhi walipelekwa Serian hospital kwa matibabu, majeruhi wanne wameruhusiwa na watatu wamelazwa na wanaendelea vizuri."
Chanzo-Kibonajoro.com

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post