News Alert_TFF YAMTIMUA KOCHA MKUU WA TIMU YA TAIFA MAART NOOIJ,BENCHI LA UFUNDI LAVUNJWA PIA

stars
Baada ya kufungwa mfululizo kwa timu ya Taifa, Taifa Stars hatimaye kocha mkuu wa timu hiyo Maart Nooij ametimuliwa kazi ya kuendelea kukinoa kikosi hicho.


Kamati ya utendaji ya Shirikisho la soka Tanzania TFF katika kikao chake kilichokaa jana usiku kimefikia uamuzi huo wa kumsimamisha kazi kocha huyo kuanzaia leo June 21 pamoja na kuvunja benchi la ufundi la timu hiyo.

TFF imeahidi kutangaza wakati wowote benchi  jipya la ufundi la timu hiyo.

Stars iliambulia kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Uganda jana katika uwanja wa Amaan ikiwa ni mechi ya kwanza ya kufuzu mashindano ya CHAN 2016 yatakayofanyika Rwanda.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post