News Alert_ MBUNGE MWINGINE AFARIKI DUNIA TANZANIAMbunge wa jimbo la Geita Donald Max amefariki dunia leo jioni ya Juni 23, 2015 katika hospitali ya Taifa Muhimbili. 

Katibu wa bunge Dr Thomas Kashilila amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kwamba taarifa zaidi zitatolewa kesho Juni 24, 2015.

Msiba huu unatokea ikiwa ni wiki tatu tangu kufariki kwa mbunge wa jimbo la Ukoga Eugen Mwaiposa aliyefariki Juni 2 mwaka huu na takriban miezi mitatu tangu kufariki kwa mbunge wa Mbinga Magharib Kapten John Komba.

Chanzo-EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post