JANUARI MAKAMBA NAYE ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS,SAUTI IKO HAPA SIKILIZA
January Makamba akitangaza nia ya Urais leo.
June 07 2015 mmoja kati ya Viongozi ambao wameingia kwenye headlines za kutajwa kwamba na yeye anahitaji kusogelea njia ya kuingia Ikulu ya TZ kwenye Uchaguzi wa mwaka huu 2015 ni Naibu Waziri, January Makamba.
 
Tayari kathibitisha kwamba ana lengo hilo, kutoka Mlimani City Dar hapa nina nukuu ya baadhi ya sentensi zake wakati akitangaza nia hiyo.

“Nimeona nitumie siku ya leo kuwajulisha kwamba nimeamua kuomba nafasi ya Rais wa Tanzania… keshokutwa nitakwenda Dodoma kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya CCM ili niteuliwe kugombea mwaka huu.. Naelewa kiu ya Watanzania kupata aina mpya ya uongozi utakaotoa matumaini mapya yatakayozaa Tanzania mpya“>>>

“Siko mbele yenu leo kuwasimulia matatizo ya Watanzania.. niko mbele yenu kueleza tutakavyotatua matatizo ya nchi yetu. Nitaunda Serikali ya Mawaziri wasiozidi 18, haitakuwa na mtu hata mmoja anaetiliwa shaka kuhusu uadilifu wake wala uwezo wake“>>>

“Kwenye Serikali yetu tutataka kila mtu afuate Sheria za nchi hata ziwe ndogo kiasi gani.. Tutakabiliana na tatizo la ubadhilifu wa mali za umma kwa nguvu zetu zote“>>>

“Viongozi wengi wa siasa wameliita tatizo la ajira kuwa ni bomu lakini kulielezea tatizo la ajira sio kulitatua.. tukiwezesha 80% ya biashara ndogondogo hapa nchini zitakuwa zimepunguza kama sio kumaliza kabisa tatizo la ajira”>>>

“Tutaongozwa na dira ya elimu inayochochea vijana kujiajiri“>>>

“Ualimu ni wito, hatutaki ualimu uwe adhabu.. Tutazitatua changamoto za Walimu, hatutaingiza Siasa kwenye elimu“>>>– January Makamba.

 Hotuba ya January Makamba iko hapa mtu wangu, ukiplay utaisikia yote kama ulipitwa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post