ISHU YA MAKALIO NA MANYONYO YA BANDIA YATUA BUNGENI,MBUNGE ESTHER BULAYA KAFUNGUKAKwa mara nyingine tena ishu ya vipodozi imeingia kwenye mjadala wa Bunge… May 27 2015 nilikusogezea stori toka Bungeni, Wabunge wakataja majina ya ‘mikorogo’ ambayo sikuwahi kuyajua.

Leo JUNE 09 2015 Mbunge Esther Bulaya kapata kama dakika moja hivi kabla Bunge halijaahirishwa, akatoa sentensi hizi tano kuhusu ishu ya wanawake kutumia makalio na maziwa ya bandia: “Kuna tatizo kubwa limeingia kwa watu kuweka makalio ya bandia na manyonyo bandia.. Tatizo hili ni kubwa, kuna picha zinasambaa kwenye mitandao, athari yake watu wanapata cancer na kuharibika miili yao kutoka majeraha makubwa“>>>
bulaya-akitoa-maoni
Mbunge Esther Bulaya.

“Serikali isiangalie suala tu la vipodozi na mikorogo usoni.. hili la watu kuweka makalio na matiti bandia limeingia na linaleta madhara makubwa sana hasa cancer“>>>– Esther Bulaya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post