IDADI YA WATU WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA MOTO KWENYE KITUO CHA MAFUTA SASA 175

damu


Ripoti ya jana Alhamis ilionyesha idadi ya watu 96 kupoteza maisha kutokana na ajali ya moto iliyotokea katika kituo cha mafuta katika mji mkuu wa Accra Ghana.
magar
Baadhi ya magari yaliyokuwa katika kituo hicho yakiwa yameungua kabisa

Hii ni idadi ya vifo ambayo imeonyesha kuongeza ambapo mpaka sasa watu waliofariki wamefikia 175 kutokana na ajali hiyo.
ghana
Moto huo uliozuka siku ya jumatano usiku wakati wakazi wa mji huo walipokuwaeneo hilo wakijikinga na mvua kubwa ambayo imewaacha raia wengi bila makaazi pamoja na kukosekana kwa umeme kwa muda mrefu.
damu
Lori ambalo limebeba miili ya watu waliokufa kwenye moto huo likichuruzisha damu
Serikali ya Ghana imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia vifo hivyo.

mmoja
Mmoja wa majeruhi akisimulia ajali hiyo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post