Hii Nayo Kali!! SHEREHE YA KULA NYAMA YA MBWA YAANZA KUFANYIKA, MBWA 10,000 WATACHINJWA JUMAPILI WIKI HII

null


Sherehe ya kula nyama ya mbwa kusini magharibi mwa China imeanza huku kukiwa na pingamizi miongoni mwa wanaharakati wa haki za wanyama.

Takriban mbwa 10,000 watachinjwa na nyama yao kuliwa katika sherehe hizo zitakazofanyika katika eneo la Yulin mkoa wa Guangxi siku ya Jumapili na Jumatatu ili kuadhimisha kuanza kwa msimu wa joto kulingana na vyombo vya habari vya kitaifa.
 null
Mwalimu mmoja aliyestaafu kutoka Tianjin aligonga vyombo vya habari alipowanunua mbwa wengi ili kuwanusuru.

Wakaazi na wafanyibiashara huko Yulin wanasema kuwa wanyama hao huuawa kwa njia nzuri.
 
 Wanaharakati wanasema kuwa mauaji hayo ni ya kikatili na kwamba kampeni ya mitandaoni ya kupiga marufuku sherehe hiyo imetiwa sahihi na zaidi ya watu milioni 3.8 kufikia sasa na kampeni hiyo kuungwa mkono na watu wengi mwaka huu kutoka watu maarufu wa kitaifa na kimataifa.

Watu maarufu akiwemo mcheshi wa Uingereza Ricky Gervais wamezungumza katika mtandao wa Twitter na alama ya reli StopYuLin2015.
 null
Nyota wa muziki nchini Uchina Chen Kun na msanii Yang Mi wamesema kuwa wanaiunga mkono kampeni hiyo katika mtandao wa Weibo.
Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post