Hii Kali!! NABII AZIKWA AKIWA HAI ,ETI ANAONDOA MAPEPO YALIYOSHINDIKANA.. KILICHOFUATA NI STORI....

bury

Nimekutana na stori hii kutoka Zimbabwe inamhusu Nabii mmoja kutoka nchi hiyo kufariki akiwa kwenye mishemishe za kupata nguvu za ziada ili akemee mapepo.

Nabii huyo Shamiso Kanyama alifuatwa na familia moja wakamuomba aje nyumbani kwao ili afanye maombezi kuondoa mapepo yaliyokuwepo kwenye nyumba ya wanafamilia hao.

Nabii huyo akaenda kufanya maombezi na wanafamilia hao… Wakiwa katika maombezi hayo, nabii huyo alidai kuwa roho mtakatifu amezugumza nae na kuwaomba wanafamilia hao kuchimba kaburi nje ya nyumba ili wamzike akiwa hai, alafu akifufuka atakuwa na nguvu mpya ya kuendelea na maombezi hayo.

Baada ya kuona nabii huyo hatoki kaburini, wanafamilia hao wakaamua kufukua kaburi ili kumtoa nabii huyo na ndipo walipogundua kuwa tayari amefariki.


Wanafamilia hao wamekamatwa na wameshitakiwa kwa kosa la mauaji.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post