ANGALIA PICHA- TGNP MTANDAO YATOA MAFUNZO KWA WATIA NIA ZAIDI YA 70 WA UBUNGE NA UDIWANI SHINYANGA



Hapa ni katika Ukumbi wa Papa John wa pili uliopo katika kanisa la Mama Mwenye Huruma Ngokolo mjini Shinyanga ambapo jana Juni 12,2015 mafunzo ya siku 5 ya wagombea watarajiwa ngazi ya udiwani na ubunge katika uchaguzi mkuu ujao nchini Tanzania yamehitimishwa.

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na TGNP Mtandao yamekutanisha watia nia zaidi ya 70 kutoka kata na majimbo mbalimbali ya uchaguzi mkoani Shinyanga yakijumuisha washiriki kutoka vyama mbalimbali vya siasa.Mratibu wa mafunzo hayo katika mkoa wa Shinyanga ni bi Cressida Mwamboma kutoka TGNP Mtandao.
Mtia nia ya Ubunge jimbo la Shinyanga mjini kupitia CHADEMA bi Siri Yasin akizungumza wakati wa semina hiyo iliyolenga  kuwawezesha wanawake,vijana na walemavu waweze kugombea katika uchaguzi mkuu ujao,ambapo wamepatiwa mafunzo kuhusu namna ya kujenga hoja,kuelewa haki zao kutenda haki kwa kuzingatia usawa wa kijinsia kupitia makundi mbalimbali katika jamii.

Watangaza nia kuwania ubunge na udiwani kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Shinyanga

Watangaza nia makundi ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu wakiwa ukumbini wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Watangaza nia kuwania ubunge na udiwani wakiwa ukumbini,ambapo wamejengewa uwezo na maafisa kutoka TGNP Mtandao kuhusu mambo ya uongozi


Bwana Marco Mashauri ambaye ni mlemavu wa macho/asiyeona alitengaza nia kuwania udiwani katika kata ya Mhongolo akizungumza katika semina hiyo ambapo aliwataka watanzania kutowabeza watu wenye ulemavu hivyo wawape nafasi ya kuwaongoza kwani elimu na uwezo wanao
Washiriki wa semina hiyo wamefundishwa namna ya kufanya kazi na waandishi wa habari na katika harakati zao
Yohana Richard Mpongo ambaye ni mlemavu wa macho aliyetangaza nia ya kuwania udiwani katika kata ya Bugayambelele katika manispaa ya Shinyanga akizungumza katika semina hiyo ambapo aliitaka jamii kuwapa kipaumbele watu wenye ulemavu kwani nao wana haki ya kuwa viongozi kikatiba.
Mtia nia kuwania ubunge katika jimbo la Solwa bwana Moshi Enos akizungumza katika semina hiyo,kushoto ni mwandishi wa habari kutoka radio Faraja Veronica Natalis
Mtangaza nia kuwania udiwani katika kata ya Ukenyenge wilayani Kishapu John Lugembe ambaye ni mlemavu wa viungo akizungumza katika semina hiyo ambapo aliwataka wananchi kuwapa nafasi watu wenye ulemavu katika uongozi
Mtangaza nia kuwania ubunge jimbo la Shinyanga mjini kupitia CHADEMA Zenna Mussa Gulam akizungumza katika semina hiyo
Watangaza nia wakiwa ukumbini,kushoto ni Clara John aliyetangaza nia kuwania ubunge jimbo la Msalala kupitia chama cha TADEA  
Watangaza nia wakiwa ukumbini
Watangaza nia wakiwa ukumbini


Watangaza nia wakiwa ukumbini


Watangaza nia wakiwa ukumbini

Watangaza nia wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Mwezeshaji wa mafunzo hayo Sophia Ndibalema akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo


Mtangaza nia ya udiwani Charles Kafuku ambaye ni mlemavu wa viungo akionesha mpango kazi aliouandaa ili kufanikisha malengo yake
                               Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post