TUMBILI AZALIWA NA KUPEWA JINA LA MTOTO WA MFALME,KILICHOFUATA NI STORI!!

Tumbili mwenye jina sawa na binti mfalme
Hifadhi moja ya wanyama huko Japan imelazimika kuomba radhi baada ya wahudumu wake kumpa tumbili mtoto wa  kike, jina sawa na lile la mwanawe mwanamfalme wa Uingereza Charlotte.

Kituo hicho cha wanyama cha Takasakiyama kilicho kusini mwa taifa hilo kilikabiliwa na gadhabu kuu ya watu baada ya kumpa tumbili huyo wa kike jina hilo sawa na binti mfalme wa Uingereza.

Chombo cha habari cha Kyodo kiliripoti tukio hilo kikidai kuwa raia waliihusika katika kuchagua jina la tumbili huyo wa kike.

''ni kawaida kwa tumbili wa kwanza kila mwaka kupewa jina na umma'' Kyodo
Jina hilo la Charlotte ndilo lililotokea kupendwa na watu wengi huku watu 59 kati ya raia 853 wakiipigia kura.

Baadhi ya raia walipinga pendekezo hilo wakisema haifai kuipa tumbili huyo jina sawa na binti mfalme.

Wengine walisema kuwa haitakuwa vyema kwao wenyewe iwapo waingereza wataita tumbili wao majina sawa na ya wafalme wao.

Kituo hicho cha Wanyama kilichapisha taarifa kwenye mtandao wao wakiomba msamaha huku wakipanga mikakati ya kubadilisha jina la tumbili huyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post