WAZIRI WA ARDHI,NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI AWEKA JIWE LA MSINGI NYUMBA 50 ZA GHARAMA NAFUU ZA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA KAHAMAHizi ni miongoni mwa nyumba 50 za gharama nafuu zilizojengwa na shirika la nyumba la taifa (NHC) katika mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula katika halmashauri ya Mji Kahama mkoani Shinyanga.Leo Mei 29,2015 Waziri wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya makazi nchini William Lukuvi ameweka jiwe la msingi katika nyumba hizo.

Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,ndugu Kadama Malunde alikuwepo eneo la tukio,ametuletea Picha 25 za tukio zima,ANGALIA HAPA CHINI

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi nchini William Lukuvi(aliyevaa miwani) akiweka jiwe la msingi katika nyumba hizo zilizojengwa na NHC wilayani Kahama mkoani Shinyanga  

Kaimu mkurugenzi wa Uendelezaji Miliki kutoka Shirika la nyumba la taifa Haikamen Mlekio akitoa maelezo kwa waziri Lukuvi kuhusu mradi huo wa nyumba 50 wilayani Kahama ulioanza kujengwa mwezi Januari mwaka 2015 na kutarajiwa kukamilika mwezi Desemba 2015.

Mradi huo wa nyumba 50 utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 2.1 na kila nyumba ina vyumba vitatu. 

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi nchini William Lukuvi akikata utepe,kulia kwake ni kaimu mkurugenzi mkuu wa Shirika la nyumba la taifa Felix Maagi  

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi nchini William Lukuvi  akiwa ndani ya moja ya majengo hayo,wa kwanza kushoto ni kaimu mkurugenzi mkuu wa Shirika la nyumba la taifa Felix Maagi 
Wa pili kulia ni kaimu mkurugenzi mkuu wa Shirika la nyumba la taifa Felix Maagi akitoa maelekezo kwa waziri Lukuvi baada ya kukagua moja ya majengo hayo 50 yaliyojengwa na NHC
Meza kuu-Lengo la NHC  kujenga nyumba ni kuleta mvuto kwa miji yetu,kupandisha hadhi ya maeneo lakini pia kuwapatia wananchi wa kipato cha chini nyumba bora na gharama nafuu

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi nchini William Lukuvi akiteta jambo na mbunge wa jimbo la Kahama mjini James Lembeli 
Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson akizungumza eneo la tukio.Alilipongeza shirika la nyumba la taifa kwa kujenga nyumba za kisasa na imara,huku akipongeza pia kitendo cha NHC kutoa msaada wa mashine za kufyatulia matofali katika halmashauri za wilaya

Eneo la tukio
Kaimu mkurugenzi mkuu wa Shirika la nyumba la taifa Felix Maagi akizungumza eneo la tukio,alisema mradi huo wa nyumba za Kahama ni muendelezo wa utekelezaji wa mpango wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu nchini  ikiwa ni miongoni mwa maeneo 29 ya halmashauri mbalimbali za miji.

Kaimu mkurugenzi mkuu wa Shirika la nyumba la taifa Felix Maagi, alisema mradi huo wa umetengeza ajira za moja kwa moja 290,ajira shirikishi 145,makazi ya watu 300 na utanufaisha wananchi wa Kahama wakiwemo wafanyabiashara. 

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi nchini William Lukuvi akiwahutubia wakazi wa Kahama katika eneo la mradi wa nyumba 50 zilizojengwa na shirika la nyumba la taifa (NHC) katika mtaa wa Bukondamoyo kata ya Mhungula wilayani Kahama.
Tunamsikiliza waziri Lukuvi....
Waziri Lukuvi pamoja na mambo mengine alizitaka halmashauri za wilaya kupima maeneo ya miji na kuyagawa kwa wananchi kwa utaratibu unaotakiwa ili kuondoa migogoro ya ardhi na kuweka mipango ya miji vizuri.
Wananchi wakimsikiliza waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi nchini William Lukuvi,ambaye alisema wananchi watakaonunua nyumba za shirika la nyumba la taifa hivi sasa kuna utaratibu wa kupatiwa hati miliki hata kama nyumba iko juu ya ghorofa ili kuwarahisishiwa kupata mahitaji mengine muhimu ikiwemo mikopo.
 
Tunafuatilia kinachoendelea.....
Kundi la sanaa la Makhirikhiri wa Kahama wakitoa burudani

Nyumba moja inauzwa shilingi milioni 49 na tayari watu mbalimbali wamejitokeza kununua nyumba hizo za kisasa
Kundi la Makhirikhiri likitoa burudani
Kiongozi wa kundi la sanaa la Makhirikhiri Kahama akishikana mkono na viongozi akiwemo Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi nchini William Lukuvi 
 Wananchi wakiwa eneo la tukio
Mbunge wa jimbo la Kahama Mjini James Lembeli akizungumza katika eneo la mradi ambapo aliwataka wakazi wa Kahama kuchangamkia fursa ya nyumba hizo kwa kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ya kibiashara katika eneo hilo ili fedha za watu watakaoishi hapo zisitoke nje ya eneo hilo.

Wananchi wakiwa eneo la tukio
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post