TBS YAWATAKA WANANCHI KUKAGUA BIDHAA WAKATI WA KUZINUNUA


Mei 30,2015-Hapa ni katika Banda la Shirika la Viwango nchini (TBS),mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya 13 ya Viwanda Vidogo Kanda ya ziwa  yaliyoandaliwa na ,kwa niaba ya waziri wa Viwanda na Biashara nchini,yanayofanyika katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga akishikana mkono na Ofisa Mahusiano wa Shirika la Viwango nchini (TBS),Roida Andusamile alipotembelea banda hilo.

Ofisa Mahusiano wa Shirika la Viwango nchini (TBS),Roida Andusamile,akizungumza katika Banda la TBS  mbele ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambapo aliwataka watumiaji wa bidhaa mbalimbali hapa nchini kujenga mazoea ya kukagua ubora wa bidhaa wanazozinunua kabla ya kuzinunua ili kuhakikisha iwapo zimekaguliwa na kuwekewa alama ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Andusamile alisema tabia ya matumizi ya bidhaa zisizo na viwango ina madhara makubwa kwa mtumiaji hasa upande wa vyakula ambavyo humsababishia mlaji matatizo ya kiafya na hivyo kulazimika kutumia fedha nje ya bajeti yake kwa ajili ya kutafuta matibabu.



 Ofisa Mahusiano wa Shirika la Viwango nchini (TBS),Roida Andusamile,alisema bado kuna changamoto nyingi hapa nchini juu ya suala zima la uhakiki wa ubora wa bidhaa ,kwani wapo wafanyabiashara wasio waaminifu wanaopenyeza bidhaa zenye kiwango cha chini na kuziingiza ndani ya soko ambapo matumizi ya bidhaa hizo ni hatari kwa afya ya walaji.

Wakazi wa Shinyanga pia walifika katika banda hilo la TBS na kupata elimu kuhusu mambo mbalimbali yanayofanywa na TBS

Ofisa Mahusiano wa Shirika la Viwango nchini (TBS),Roida Andusamile akitoa elimu kwa wakazi wa Shinyanga-Alisema ili wananchi waweze kufaidika na viwango vya bidhaa mbalimbali, Shirika lake linaendesha mpango wa uthibiti wa ubora wa bidhaa, ambao unaliwezesha shirika kutoa leseni kwa wazalishaji bidhaa wanaothibitishwa kuwa wazalishaji kulingana na kiwango cha kitaifa cha bidhaa husika ambayo huwaruhusu kutumia alama ya “TBS” ya ubora wa bidhaa.

Ofisa Mahusiano wa Shirika la Viwango nchini (TBS),Roida Andusamile,alisisitiza juu ya umuhimu wa wananchi kukagua bidhaa wanazonunua kwa kuangalia kama zina alama ya TBS huku wakishiriki kuwafichua watu wanaozalisha bidhaa zisizokuwa na kiwango ili kuondokana na bidhaa hafifu sokoni.

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 Blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527