Angalia Picha!! AGPAHI YAZINDUA MAJENGO YA HUDUMA ZA TIBA NA MATUNZO KWA WATU WANAOISHI NA VVU SHINYANGA



Shirika la AGPAHI (Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative) linalojihusisha na mapambano dhidi ya ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI linalofadhiliwa na watu wa Marekani kupitia Shirika la Kimarekani la Center for Disease Control and Prevention(CDC) nchini Tanzania leo limezindua majengo mawili kwa ajili ya  Huduma za Tiba na Matunzo kwa watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI katika zahanati ya Kagongwa wilayani Kahama na kituo cha afya cha Nindo kilichopo katika wilaya ya Shinyanga Vijijini Mkoani Shinyanga.

Majengo hayo yamezinduliwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga ambapo alisema serikali ya mkoa wa Shinyanga inatambua sana mchango wa shirika la kitanzania la AGPAHI linalofanya kazi zake katika mkoa huo na mikoa ya Geita na Simiyu katika jitihada zake za kupambana na VVU.

Mbali na kupongeza kazi nzuri inayofanywa na AGPAHI,Rufunga alisema majengo hayo ya kisasa yatakuwa msaada mkubwa katika kutoa huduma ya tiba na matunzo kwa watu wote walio na maambukizi ya VVU na UKIMWI,pia huduma ya kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Naye mkurugenzi mtendaji wa AGPAHI Lauren Rugambwa Bwanakunu alisema katika mkoa wa Shinyanga kuna vituo 43 vinavyotoa huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU na UKIMWI na vituo 310 vinavyotoa huduma za kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto katika mikoa ya Shinyanga,Simiyu na Geita.

Bwanakunu alisema lengo la kujenga majengo hayo ni kuondoa msongamano wa wateja na kuongeza ubora wa huduma na usiri.

Shirika la AGPAHI lilianza kazi zake mwaka 2011 kwa msaada wa watu wa Marekani kwa kusaidiana na serikali ya Tanzania.

Shirika la AGPAHI limetokana na shirika la kimataifa la EGPAF,lililokuwa likisaidia upatikanaji wa huduma na matunzo kwa watu wenye VVU. 

Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo wakati wa Uzinduzi wa Majengo hayo mawili katika zahanati ya Kagongwa wilayani Kahama na kituo cha afya cha Nindo katika wilaya ya Shinyanga vijijini,Ametuletea picha 50 Tazama hapa chini

KAZI ILIANZIA KWENYE ZAHANATI YA KAGONGWA
Hili ni jengo la huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU na UKIMWI katika zahanati ya Kagongwa lililopo katika halmashauri ya mji Kahama,limejengwa na Shirika la AGPAHI linalofadhiliwa na watu wa Marekani kupitia Shirika la Kimarekani la Center for Disease Control and Prevention(CDC).

Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe akizungumza wakati wa uzinduzi huo ambapo alisema uwepo wa jengo hilo utasaidia wakazi wa eneo hilo na maeneo ya jirani kuwa na ari ya kupima afya zao na kupata matibabu mbalimbali.

Dkt Kapologwe alisema mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa yenye ushamiri mkubwa wa maambukizi ya VVU na UKIMWI ambapo sasa maambukizi ni asilimia 7.4.

Mkurugenzi mtendaji wa AGPAHI Lauren Rugambwa Bwanakunu akizungumza katika zahanati ya Kagongwa ambapo alisema zahanati hiyo ni kati ya vituo 43 vinavyopata misaada katika huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU.
Alisema misaada inayotolewa na AGPAHI ni pamoja na vitendea kazi(pikipiki),vifaa vya ofisi(viti,meza,kabati,computer,printer n.k


Tunafuatilia kinachoendelea hapa……..
Mkurugenzi mtendaji wa AGPAHI Lauren Rugambwa Bwanakunu alisema pia AGPAHI kwa kushirikiana na wizara ya afya inawajengea uwezo watumishi wa afya kwa njia ya mafunzo.

Misaada mingine inayotolewa na AGPAHI ni vifaa tiba(BP Mashine,PIMA Machine,Statoscope,mizani na madawa.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya akizungumza wakati wa uzinduzi huo ambapo aliwataka wakazi wa Kahama na maeneo ya jirani kujitokeza kwa wingi kupata huduma zinazotolewa katika zahanati ya Kagongwa ambayo baadaye itapandishwa hadhi na kuwa kituo cha afya.
Kikundi cha maigizo kikitoa somo na burudani
Jengo hili lina vyumba 7 vya kutolea huduma na sehemu ya kusubiria.Vyumba vine ni vya waganga,kimoja cha dawa,kuna cha nasaha na kingine ni masjala.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akizindua/akifungua jengo hilo.
Kilichokuwa kinasomeka ukutani-Zahanati hiyo pia imeweza kuwaanzishia dawa wateja wapatao 1,819( wanaume 716 wanawake 1,103) ,na kwenye matunzo kati yao watoto ni 129 sawa na 7%.

Mkurugenzi mtendaji wa AGPAHI Lauren Rugambwa Bwanakunu akishiriki uzinduzi wa jengo hilo.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akijiandaa kukata utepe
Tabibu wa zahanati ya Kagongwa James Bundala akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga katika chumba cha masjala katika jengo hilo.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akiwa katika chumba cha Nasaha katika jengo la Huduma za Tiba na Matunzo kwa watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI katika zahanati ya Kagongwa wilayani Kahama.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akisisitiza jambo katika moja ya vyumba vya jengo hilo la kisasa.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga na viongozi mbalimbali wa mkoa,wilaya na AGPAHI wakielekea jukwaa kuu baada ya kuzindua jengo hilo.
Watumishi wa zahanati ya Kagongwa wakicheza
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akitoa hotuba yake ambapo alitoa wito kwa wazazi ambao watoto wao wamepatwa na maradhi ya UKIMWI wawapeleke kuwaandikisha pia wao wenye kujiandikisha kwenye huduma zinazotolewa katika kituo hicho na kuhudhuria kliniki mara kwa mara.

Wakazi wa Kagongwa wakiwa eneo la tukio
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akizungumza wakati wa uzinduzi huo ambapo alisema AGPAHI wamekuwa msaada mkubwa kwa katika utoaji huduma za afya mkoani Shinyanga.

Watumishi katika zahanati ya Kagongwa wakiwa wamesimama-Hawa ni miongoni mwa watumishi walionufaika na mafunzo mbalimbali yanayotolewa na AGPAHI katika kuwajengea uwezo kuhusu mambo ya afya.

Hadi mwezi Machi 2015,zahanati ya Kagongwa imeweza kuandikisha wateja 3001( wanaume 1,155 na wanawake 1,846) kati yao watoto ambao wako chini ya miaka 15 ni 186 sawa na 6.2%.

Picha za pamoja na mkuu wa mkoa wa Shinyanga zikaanza kupigwa

Upigaji picha za pamoja Unaendelea

Picha ya kumbukumbu
KAZI IKAENDELEA KATIKA WILAYA NYINGINE_HAPA NI KATIKA WILAYA YA SHINYANGA VIJIJINI KATIKA KITUO CHA AFYA NINDO UZINDUZI WA JENGO UMEFANYIKA PIA.
Hili ni jengo la Huduma za Tiba na Matunzo kwa watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI katika cha afya cha Nindo kilichopo katika kata ya Iselamagazi wilaya ya Shinyanga Vijijini Mkoani Shinyanga,ambalo pia lina vyumba 7  kama jengo la zahanati Kagongwa wilayani Kahama.

Katibu tawala wilaya ya Shinyanga Boniface Chambi kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo hilo ambapo aliliomba shirika la AGPAHI kuendelea kutoa msaada kwa wakazi wa Shinyanga kwani wanapata manufaa mengi.

Mbunge wa jimbo la Solwa Ahmed Salum akizungumza wakati wa uzinduzi huo ambapo alipongeza kazi ya AGPAHI katika kuwafikia wananchi huku akitoa ahadi ya kuendelea kushirikiana na shirika hilo katika kujali afya za wakazi wa jimbo lake.

Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe akizungumza katika kituo cha afya cha Nindo.
Hadi kufikia mwezi Machi,2015,kituo cha afya cha Nindo kimeweza kufikiwa na wateja 1379( wanaume 532,wanawake 847) na kwenye huduma ya matunzo kati yao watoto ni 80 walio chini ya miaka 15 sawa na 6%.

Hiki ni choo kilichojengwa na AGPAHI katika kituo cha afya cha Nindo katika wilaya ya Shinyanga.

Muonekano wa jengo hilo la kisasa

Kikundi cha kwaya ya Mshikamano wakiimba wimbo kuhusu UKIMWI

Mbunge Ahmed Salum akicheza na kikundi cha wahamasishaji kuhusu masuala mbalimbali  kuhusu UKIMWI. katika kituo hicho cha afya cha Nindo.

Mkurugenzi mtendaji wa AGPAHI Lauren Rugambwa Bwanakunu akizungumza katika kituo cha afya cha Nindo ambapo aliwataka wanaume kubadili tabia na kuwa tayari kupimwa afya zao wakiwa pamoja na wenzi wao ili kuzuia maambukizi ya VVU kwa watoto wanaozaliwa kwani baba na mama watakuwa wanajua afya zao kabla ya kuamua kupata mtoto.

Jukwaa kuu, tunafuatilia kinachoendelea....

Wakazi wa Iselamagazi wakiwa eneo la tukio

Mkurugenzi mtendaji wa AGPAHI Lauren Rugambwa Bwanakunu akifurahia jambo na mbunge Ahmed Salum

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akizindua jengo katika kituo cha afya cha Nindo lililojengwa kwa ufadhili wa  Centers For Desease Control and Prevention

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akikata utepe katika jengo hilo

Sista Emelda Misana,ambaye ni muuguzi mkunga katika kituo cha afya cha Nindo akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga  Ally Rufunga katika chumba cha nasaha.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akiangalia TV iliyopo katika eneo la kusubiria huduma katika kituo cha afya cha Nindo wilaya ya Shinyanga vijijini.

Wanenguaji wa kikundi cha Ukombozi kinaimba nyimbo za asili wakifanya yao

Burudani inaendelea

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga akitoa hotuba yake
ambapo aliwataka viongozi wa wilaya kuhakikisha kuwa majengo hayo yanatunzwa na kufanyiwa ukarabati ili yaweze kudumu kwa muda mrefu.

Baada ya uzinduzi ,picha za kumbukumbuku

Picha za kumbukumbuku

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527