MSWAADA WA VYOMBO VYA HABARI WAZUA BALAA,MOAT YAUNDA KAMATI KUWASHAWISHI WABUNGE WASIUPITISHE!!

Chama cha wamiliki wa vyombo vya habari nchini -MOAT kimeunda kamati maalum ya kuwashawishi wabunge ili wasiupitishie mswaada wa vyombo vya habari kuwa sheria, baada ya kubaini kuwa unakusudia  kufinya uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa wananchi kupata habari na utaua vyombo vya habari vya binafsi.



Maamuzi ya kuunda kamati hiyo yametolewa jijini Dar es Salaam baada ya wamiliki wa vyombo vya habari nchini kukutana na kupata ufafanuzi wa kisheria kuhusu muswada huo kutoka kwa mwanasheria wao Bw. Godfrey Mpandikizi.
Akizungumza mwenyekiti wa MOAT Dr Reginald Mengi amesema Tanzania inasifika duniani kwa amani, uwazi, na kwa kuwa na uhuru wa vyombo vya habari, lakini sifa hizo zinaweza kufutika kama muswada huo utapitishwa, hususan wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu.
Kabla ya kutoa maazimio hayo baadhi ya wanachama walitopata fursa ya kuchangia mawazo walisema muswada huo wa sheria una nia mbaya kwa tasnia ya habari na ni kinyume cha katiba ya nchi.

Katika hatua nyingine wakati wizara ya mawasiliano Sayansi na Teknoljia ikiwasilisha bajeti ya wizara yake bungeni mjini Dodoma, baadhi ya wabunge wamepinga vikali sheria mbalimbali ambazo serikali imezipitisha ikiwemo ya miamala ya kieletoniki ya mwaka 2015 na sheria nya udhibiti wa uhalifu wa mtandao wa mwaka 2015 kuwa inafifisha uhuru wa watu kutoa taarifa mbalimbali ambazo zingeweza kusaidia kuharakisha maendeleo katika nchi.


Akiwasilisha bajeti ya wizara yake Mh Profesa Makame Mbarawa amesema wizara yake itahakikisha inaendelea kusimamia kwa kina sheria zilizopo ili kuona kuwa tekinolojia haitumiki vibaya.
 
 
 
Akizungumza kuhusu sheria hizo Mh Mchungaji Peter Msigwa amesema inashangaza kuona ni katika kipindi muhimu kama hiki ambacho watu wanahitaji kupata taarifa nyingi tena za uhakika alafu serikali inabinya uhuru wa wawatu kupata taarifa hizo.
 
 
 
Awali waziri wa viwanda na biashara Mh Abdallah Kigoda akiwasilisha bajeti ya wizaya yake amesema serikali inakusudia kutoa leseni kwa wamachinga wote ili waweze kufanya biashara katika mazingira tulivu. 
 
 
 
Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa kamati ya bunge uchumi na biashara Mh Dunstan Kitandula amesema licha ya jitihada zinazofanywa na wizara lakini bado kuna tatizo kubwa katika uwepo wa viwanda nchini jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya nchi.
 
Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527