Kashfa Jeshi la Polisi!! WATEKA MAAFISA WA SERIKALI,WAWAPORA MAMILIONI YA FEDHA WAKIGOMBEA MALI HARAMU!!

Askari Polisi saba akiwemo mkuu wa kituo cha Polisi Murongo wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera Bw.Richard Msusi wanatuhumiwa kupora fedha zaidi ya shilingi milioni saba baada ya kuwateka nyara maafisa wa halmashauri ya wilaya ya Kyerwa wakitumia bunduki na mabomu eneo la Murongo katika mpaka wa Tanzania na Uganda wakigombea kukagua gari lenye shehena ya bidhaa ambazo haziruhusiwi kuingia hapa nchini.


Maafisa wa halmashauriya wilaya ya Kyerwa baada ya kuachiwa huru na jeshi la polisi wamesema kuwa chanzo cha kukamatwa na kuporwa fedha ni baada ya kuwazuia Polisi wasiruhusu gari lenye shehena ya bidhaa zisizoruhusiwa kuingia hapa nchini zikiwemo pombe haramu aina ya Empire zinazozalishwa nchi ya Uganda kwa madai kuwa gari hilo limekaguliwa na maafisa wa TRA na polisi kwenye mpaka wa Tanzania na Uganda hivyo halmashauri haina mamlaka ya kukagua gari hilo hali iliyosababisha mgogoro kati ya polisi na maafisa wa halmashauri.
 
 
 
Kufuatia hali hiyo mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye ni mkuu wa mkoa wa Kagera Bw.John Mongella akalazimika kwenda katika eneo la tukio ambapo akiwa njiani katika hali isiyokuwa ya kawaida barabara ya kaisho Murongo ikafungwa na vifusi vya mchanga hali iliyosababisha polisi kumsimamia mkandarasi kusambaza vifusi vya mchanga ili kuruhusu msafara wa mkuu wa mkoa upite ambapo katibu wa CCM wilaya ya Kyerwa Bi.Odilia Maholelo ameshangazwa na kitendo cha kufungwa barabara inayotumika.
 
 
 
Baada ya barabara kufunguka msafara ukaendelea ambapo mkuu wa mkoa wa Kagera Bw.John Mongella akaitisha kikao cha kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Kyerwa na baadaye akazungumza na ITV akisema kwamba ofisi yake inachunguza kwa kina tuhuma  hizo na atakayebainika kukiuka sheria za tumishi wa umma atawajibishwa kisheria.
 
Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527