Rais
wa Msumbiji Mhe Filipe Nyussi amewasili nchini Tanzania kuanza ziara
yake ya kikazi ikiwa ni ziara yake ya kwanza kuifanya hapa nchini tangu
achaguliwe kuwa rais wa nchi hiyo.
Rais wa Msumbiji Filipe Jasinto Nyussi amepokelewa na mwenyeji wake
rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Mrisho Kikwete
ambapo baada ya utambulisho kwa baadhi ya viongozi waliojitokeza
kumpokea rais huyo nyimbo za taifa zikiimbwa.
Nyimbo hizo ziliambatana na upigwaji wa
mizinga kisha rais Nyussi akapata nafasi ya kukagua gwaride maalum
lililoandaliwa kwaajili yake huku shamrashamra za shangwe na burudani ya
ngoma za asili zikionesha ukarimu wa watanzania.
Akiwa Tanzania rais Nyusi atazungumza kwa faragha na mwenyeji wake
rais Jakaya Mrisho Kikwete, kuongea na wafanyabiasha wa Msumbiji waishio
hapa nchini ambapo tarehe 18 ataendelea na ziara yake visiwani Zanzibar
kisha tarehe 19 rais Jasinto atahitimisha ziara yake mjini Dodoma kwa
kuhutubia bunge la bajeti linaloendelea mjini humo.
Via>>Itv