Makovu ya Uchaguzi Serikali za Mitaa!! WANANCHI WAVUNJA OFISI YA AFISA MTENDAJI

Wananchi wa kijiji cha Nduoni  kata ya Kirua magharibi wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wamelazimika kuvunja ofisi ya afisa mtendaji wa kijiji ambayo imefungwa kwa zaidi ya miezi sita kutokana na vurugu za kumkataa mwenyekiti aliyeapishwa kwa makosa katika uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.



Wananchi hao wamelazmika kuvunja ofisi hiyo na kumuingiza mwenyekiti aliyeshinda kihalali katika uchaguzi huo Bw.Thomas Ngowi na afisa mtendaji Camilus kessy kwa madai ya kukosa huduma muhimu kwa muda mrefu na hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya kijiji hicho.


 
Wamesema kukosekana kwa uongozi wa kijiji hicho kumesababisha miradi ya maendeleo kukwama sanjari na wananchi kulazimika kwenda katika kijiji cha jirani kutafuta huduma.
 

Akizungumza mara baada ya kufunguliwa kwa ofisi hiyo mwenyekiti wa kijiji hicho Bw.Thomas Ngowi amesema zaidi ya wananchi wapatao 2800 wamekuwa wakitaabika kwa kukosa hudumaa katika kijiji hicho na kwamba yuko tayari kufanyakazi kwa kushirikiana na mtendaji wa kijiji hicho kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo.
 

Naye afisa mtendaji wa kijiji cha Nduoni Bw.Camilius Kessy amesema mweneykiti huyo ndiye aliyechaguliwa na wananchi kihalali na kuahidi kushirikiana naye pamoja na wananchi wa kijiji hicho ili kutoa huduma  bora za kuleta maendeleo katika kijiji hicho.
Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post