Walimwengu Bwana!! WAFANYAKAZI WA MOCHWARI WAIVUA NGUO MAITI,WAIBA HADI VIATU !!Hii imeripotiwa toka Embu, Kenya.. nilipoiona nikadhani inafanana na ile ya Kibaha Tanzania ambako wezi walivunja kaburi na kuiba mabegi ya nguo ambazo marehemu aliomba azikwe nazo.. baada ya kuifatilia nikakuta hii iko tofauti kidogo, japo zote zinahusu matukio wanayofanyiwa marehemu.

Wanafamilia waligundua kuwa mwili wa marehemu ndugu yao umewekwa kwenye jeneza bila kuvalishwa nguo wala viatu ambavyo walipeleka mochwari.


Wafanyakazi wa mochwari hawakumvalisha nguo hizo,kwa lugha nyingine wahudumu wa mochwari waliiba nguo za marehemu.Inaelezwa kuwa marehemu alikuwa na nguo mpya kisha akawekwa ndani ya jeneza lakini wakati wa kutaka kuchukua mwili wa marehemu ndugu wakashtuka, kuangalia kwenye jeneza wakakuta maiti kavalishwa nguo zingine tena za mitumba.

Nguo zenyewe tulikuwa tumeleta haziko kwa mwili.. mwili umewekwa mitumba, tshirt ya mtumba, suruali ya mtumba hata viatu haikuwa imewekwa”, alisema mmoja wa ndugu wa marehemu.

Baada ya ishu hiyo kuwa na mvutano ilibidi ndugu wanunue nguo nyingine za kumvalisha ndugu yao, lakini bado walibaki na maswali ambayo hayakuwa na majibu, nguo walizoleta mara ya kwanza ziko wapi ??

Nimekuwekea taarifa hiyo iliyoripotiwa na kituo cha K24…
Kutazama video ya tukio hilo bonyeza play hapa chini…

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post