BUNDI ATUA BONGO MOVIE SHINYANGA,WASANII WAVURUGANA VIBAYA,MWENYEKITI AKAMATWA NA POLISI

Watangazaji Veronica Natalis(V2),Richard Ndariro(RND), Athanas Fabian (DJ Hunter) na msanii wa bongo movie Shinyanga aliyefukuzwa uanachama Amina Francis Mwandu wakiwa ndani ya studio ya radio Faraja fm Stereo wakati wa kipindi cha Faraja Mamboleo

Watangazaji Veronica Natalis,Richard Ndariro,DJ Hunter na msanii wa bongo movie Shinyanga aliyefukuzwa uanachama Amina Francis Mwandu


Watangazaji Veronica Natalis(V2),Richard Ndariro(RND), Athanas Fabian (DJ Hunter) na msanii wa bongo movie Shinyanga aliyefukuzwa uanachama Amina Francis Mwandu wakiwa ndani ya studio ya radio Faraja fm Stereo wakati wa kipindi cha Faraja Mamboleo

Richard Ndariro,Kadama Malunde,Veronica Natalis na Amina Mwandu


Kumekuwepo na sintofahamu baina ya wasanii katika kundi la wasanii wa kuigiza “Bongo Movie Shinyanga”,ambapo baadhi ya wasanii wa kundi hilo wakimtupia lawama mwenyekiti wa Bongo Movie Shinyanga.

Inaelezwa kuwa kinachoendelea hivi sasa ni kwamba mwenyekiti wa Bongo Movie Shinyanga Juma Ibrahimu Songoro "Songoro Gaddafi" anashikiliwa na jeshi la polisi Shinyanga kwa kosa la kumtishia kumuua aliyekuwa katibu wa Bongo Movie Shinyanga Sophia Kichochi baada ya kudai mshahara wake kutokana na kufanya kazi kwa muda mrefu bila kulipwa.

Miongoni mwa wasanii wa kundi hilo Amina Francis Mwandu anasema migogoro imeanza mwezi Machi mwaka huu baada ya Filamu ya Firigisi kumaliza kurekodiwa ambapo mwenyekiti alimfukuza katibu wake akidai kuwa anavujisha siri za ofisi baada ya hapo akamfukuza pia msanii Amina Mwandu,mhusika mkuu katika filamu ya Firigisi inayohusu mauaji ya albino ambayo hata sokoni bado haijaingia.

Katika maelezo yake Songoro anasema alimfukuza katibu wake kutokana na utovu wa nidhamu huku akikanusha kuwa siyo katibu wake bali alikuwa mfagiaji tu katika ofisi yao.

Hapa nimekurekodia Interview iliyofanyika kwenye Kipindi cha Faraja Mamboleo kinachorushwa na Radio Faraja fm ya Shinyanga kila siku Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa saba mchana.Utasikia sauti ya watangazaji Veronica Natalis(V2),Richard Ndariro (RND),DJ Hunter,msanii Dennis Sweya (Dino) wa Bongo Movie Dar es salaam director wa filamu ya Firigisi,Songoro,waandishi wa habari Kadama Malunde na Chibura Makorongo.


Sikiliza/Download hapa chini ,chagua njia moja kati ya hizi 2

BOFYA HAPA KUSOMA HABARI YA KWANZA KUCHAPISHWA NA MTANDAO HUU KUHUSU BONGO MOVIE SHINYANGA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post