Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANGALIA PICHA ZA AJALI YA BASI LA JORDAN HUKO NZEGA-TABORA,GARI LILIMSHINDA DEREVA KWENYE KONA,LIKAPINDUKA,LIKAUA

Mtu mmoja amefariki dunia  na wengine  25 kujeruhiwa baada ya basi la Jordan lililokuwa likitoka Mwanza kwenda Arusha kupinduka eneo la Nzega mkoani Tabora.
Mtu huyo mmoja aliyepoteza maisha ni baada ya kulaliwa na basi hilo.

Basi hilo lenye namba za usajili T650 AQZ, inaelezwa kuwa lilipinduka baada ya kumshinda dereva katika eneo lenye kona kali.
Baadhi ya Majeruhi mara baada ya ajali hiyo kutokea.

Baadhi ya Abiria wakiwa nje ya basi la Jordan mara baada ya kupinduka wilayani Nzega mkoani Tabora na kupelekea kifo cha mtu mmoja.

Mmoja wa abiria akifanya mawasiliano baada ya kunusurika kifo mara baada ya basi la Jordan kupinduka wilayani Nzega mkoani Tabora na kupelekea kifo cha mtu mmoja.

Pichani juu ni mmoja wa majeruhi akisaidiwa na msamaria mwema mara baada ya kupata ajali.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com