Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TAZAMA PICHA!! UFUNGUZI WA MAADHIMISHO YA WIKI YA WATAALAM WA MAABARA ZA AFYA TANZANIA KITAIFA SHINYANGA


Wataalamu wa maabara za afya kutoka nje na ndani ya mkoa wa Shinyanga wakiandamana kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga kuelekea katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga leo asubuhi wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya wataalam wa maabara za afya Tanzania yanayofanyika kitaifa mkoani Shinyanga.



Maadhimisho hayo ya 5 yameandaliwa na Chama Cha Wanasayansi wa Maabara za Afya Tanzania(Medical Laboratory Scientist Association of Tanzania-MELSAT)  wakishirikiana na ofisi ya mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga-picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog


Maandamano yanaendelea-Maadhimisho ya 5 yawiki ya wataalamu wa maabara za afya nchini yakiwa na kauli mbiu ya “Pata Majibu” yamezinduliwa kitaifa mkoani Shinyanga na yanaadhimishwa kuanzia Aprili 20,2015 hadi Aprili 25,2015 ambapo shughuli za upimaji afya za binadamu zitafanyika katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga.


Maandamano yanaendelea-Miongoni mwa madhumuni ya maadhimisho hayo ni kuongeza uelewa wa taaluma ya sayansi na maabara za afya katika jamii,kuonesha kazi za wana maabara za afya,kuhamasisha wanafunzi walio shuleni kujiunga na fani ya maabara za afya na kutambua mchango wa wataalamu wa maabara za afya ambao wameleta mafanikio katika huduma za maabara za afya pia kutathimi kazi za wana maabara za afya,kuweka mikakati mipya ya utekelezaji na kuimarisha shughuli za kanda
Mada kuu ya maadhimisho ya wiki ya wataalam wa Maabara za afya ni "Laboratory Professional Get Results"(Wataalam wa Maabara Pata Majibu) na kauli mbiu hiyo ya "Pata Majibu" inatumika kila mwaka bila kubadilika lengo kubwa likiwa ni Uongozi wa Chama cha  Wanasayansi wa Maabara za Afya Tanzania(Medical Laboratory Scientist Association of Tanzania-MELSAT) 
Mtaalam wa Maabara za afya Dr Joel kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga akiwa katika moja ya banda la vipimo vya afya ya binadamu katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga


Wataalam mbalimbali wa maabara kutoka Shinyanga hasa katika chuo cha Uuguzi cha Kolandoto na wengine kutoka nje ya mkoa wa Shinyanga wakiwa katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga
Maandamano yakafikia mwisho- Wataalam wa maabara baada ya kuhitimisha maandamano yao yaliyopokelewa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa maadhimisho hayo Kitaifa
Jukwaa kuu wakiwa wamesimama wakati wa kupokea maandamano hayo.Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na mganga mkuu wa manispaa ya Shinyanga Dr Frank Mbulinyingi

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akizungumza baada ya kupokea maandamano ya wataalamu wa maabara,ambapo pamoja na mambo mengine Rufunga alisema wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,taasisi mbalimbali za elimu na wadau wa maabara wanalo jukumu kubwa la kuboresha huduma za maabara za afya nchini kwa kuwaendeleza wana maabara kielimu kwani kujiendeleza kielimu ndiyo ufunguo wa mambo mengi katika jamii.


Rufunga alisema mtumishi anapopata mafunzo kwa kujiendeleza kielimu anakuwa na upeo mkubwa wa kufanya kazi yake kwa ufanisi mkubwa na hivyo kuboresha maslahi yake na wakati huo huo jamii inapata huduma nzuri zaidi kutoka kwa mtumishi huyo.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga  akiwa karibu na wataalamu wa maabara wakiongozwa na rais wa Chama Cha Wanasayansi wa Maabara za Afya Tanzania(Medical Laboratory Scientist Association of Tanzania-MELSAT) Sabas Mrina
Chama Cha Wanasayansi wa Maabara za Afya Tanzania(Medical Laboratory Scientist Association of Tanzania-MELSAT)  kina jukumu la kuhamasisha,kuelimisha na kusimamia maadili ya taaluma ya maabara za afya ili kuhakikisha kwamba wanachama na wataalamu wote wa maabara za afya wanazingatia weledi wa kazi zao na kutekeleza majukumu yao kwa vitendo


Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akikagua mabanda ambapo kuanzia leo Aprili 20 hadi 25,2015 ,wataalam wa maabara watafanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupima ugonjwa wa kisukari,shinikizo la damu,malaria,hali ya virusi vya Ukimwi,kutoa elimu kwa jamii,kuhamasisha kutoa damu kwa watu watakaopenda kuchangia damu au kusaidia wagonjwa na kufanya semina kwa wataalam wa maabara inayoitwa 5s KAIZEN Total Quality Management itakayo waongezea  uwezo wataalamu hao ili wafanye kazi kwa ufanisi na uadilifu zaidi.
Kulia ni Dr Bushiri Rajab ambaye ni mtaalam wa magonjwa ya Kisukari kutoka Chama cha Kisukari nchini ( TDA) pia mratibu wa magonjwa ya kisukari katika manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga juu ya ugonjwa wa Kisukari na umuhimu wa wananchi kupima afya zao


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akiendelea kutembelea mabanda.Wa pili kutoka kushoto ni mratibu wa Maabara mkoa wa Shinyanga Muhdin Hamza
Kulia ni Dr Bushiri Rajab ambaye ni mtaalam wa magonjwa ya Kisukari kutoka Chama cha Kisukari nchini ( TDA) akielezea  dalili za ugonjwa wa kisukari ikiwa ni pamoja na kiu ya mara kwa mara na unywaji wa maji mengi,kukojoa mara kwa mara mkojo mwingi,kupungua uzito kusikoeleweka licha ya kula vizuri,kutoona vizuri,kizunguzungu na uchovu wa mwili bila kufanya kazi.



Dr Rajab aliyataja matatizo ya kisukari kuwa ni kiharusi,kupooza na kupoteza kumbukumbu,upungufu wa kuona,shinikizo la damu,figo kushindwa kufanya kazi,kupungua kwa nguvu za kiume au kukosa kabisa na mengine mengi ikiwemo mshtuko wa moyo.Wa pili kutoka kushoto ni mratibu wa Maabara mkoa wa Shinyanga Muhdin Hamza


Mkuu wa mkoa akiendelea kukagua mabanda


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga akiwa ndani ya moja ya mabanda


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga baada ya kumaliza kutembelea mabanda akisisitiza jambo,kulia ni mratibu wa Maabara mkoa wa Shinyanga Muhdin Hamza
Wachezaji wa ngoma ya  Kisukuma ya Ipuja kutoka kijiji cha Ipeja wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wakionesha mbwembwe zao
Wachezaji wa ngoma ya Ipuja kutoka kijiji cha Ipeja wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wakitoa burudani katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga
Rais wa Chama Cha Wanasayansi wa Maabara za Afya Tanzania(Medical Laboratory Scientist Association of Tanzania-MELSAT) Sabas Mrina akizungumza katika maadhimisho hayo amabpo aliiomba wizara ya afya na Ustawi wa Jamii pamoja na wamiliki wa maabara za afya kutambua umuhimu wa maabara za afya katika vita dhidi ya maradhi na kuchukua hatua stahiki kuboresha mazingira ya wana maabara za afya.

Kulia ni kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dr Fabian Kalabwe akimshukuru mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga kwa kushiriki katika shughuli za ufunguzi wa siku ya maadhimisho hayo


Wataalamu wa maabara wakifuatilia kilichokuwa kinajiri


Wana maabara  wakiwa eneo la tukio



Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga alitumia fursa hiyo kuutaka uongozi wa Chama cha Wanasayansi wa Maabara za Afya Tanzania kutumia maadhimisho hayo kuleta mafanikio katika utendaji wa kazi za maabara nchini kwa lengo la kuimarisha na kuboresha huduma hizo katika taifa la Tanzania kwani huu ni wakati wa kubadilishana ujuzi na uzoefu kwa lengo la kuimarisha mbinu za utekelezaji na kuhakikisha uwepo wa ubora katika utendaji wa maabara za afya.


Miongoni mwa huduma za maabara ni kuchunguza na kuangalia afya za wananchi,kutambua uwepo wa ugonjwa katika mwili wa binadamu,kugundua magonjwa ya kuambukiza ambayo yanahitaji kuwekewa mikakati ya kuyadhibiti,kutafti magonjwa mbalimbali na kupendekeza njia za kuyadhibiti na kutoa miongozo mbalimbali ya utendaji ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kuhusu athari na mambo ya kuzingatia ili kuboresha afya za jamii-picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com