Serikali
imesema hakuna Mtanzania aliyeuawa katika matukio ya mauji ya chuki za
kibaguzi (ZENOPHOBIA) yanayofanywa na raia wa Afrika Kusini dhidi ya
wageni na tayari imeanza mpango wa kuwarudisha nyumbani watanzania 21
kati ya 23 waliohifadhiwa katika kambi mjini DURBUN nchini humo
kwa ajili ya usalama.
Akizungumza na waandishi wa habari waziri wa mambo ya nje na
ushirikiano wa kimataifa Mhe. Bernad Membe amesema vifo vya watanzania
watatu vilivyotokea nchini humo havina mahusiano na mauaji hayo
ZENOPHOBIA na kusisitiza serikali ya Afrika Kusini imeanza kuchukua
hatua na tayari watu waliohusika na kifo cha rais wa Msumbiji
wamekamatwa.
Akizungumzia idadi ya Watanzania waliohifadhiwa kwenye
Kambi katika mji wa DURBUN,Mhe Membe amesema takribani watanzania
23 wamehifadhiwa katika kambi ya Isipingo iliyo na zaidi ya raia wa
kigeni elfu tatu ambao wako chini ya ulinzi wa serikali ya Afrika Kusini
na kusisitiza serikali imeanza utaratibu wa kuwarudisha nyumbani
watanzania 21 kati yao.
Akielezea msimamo wa Tanzania kufuatia mauaji hayo ya ZENOPHOBIA
yanayoendelea nchni Afrika Kusini,Mhe. Membe amesema serikali inaungana na
jumuiya ya nchi za SADC kulaani vitendo vya mauaji yanayoendelea nchini
humo ambapo watu 8 wamekwisha uawa kikatili na kuitaka serikali ya Afrika Kusini kuzuia mauaji hayo haraka iwezekanavyo.
Aidha amesema serikali ya Tanzania haitakuwa na tatizo la
watanzania kurudi nchini humo baada ya mauaji kudhibitiwa na kwa upande
wa wafanyabishara waliosajiliwa kihalali na kupoteza mali zao, serikali
itawasiliana na wanasheria wake ili kuona namna ya kutafuta namna ya
nchi hiyo kuwafidia hasara waliyoipata.
Via>>ITV
Via>>ITV
Social Plugin