MBOWE AMJIBU IGP MANGU: "WAKIKATAZA MAFUNZO YA UKAKAMAVU KWA VIJANA,TUTAFANYA USIKU,HUU NI WIVU TU"

 

Siku moja baada ya jeshi la polisi nchini kupiga marufuku nyama vya siasa kuendelea kutoa mafunzo mbalimbali ya ukakamavu na ulinzi kwa vijana, mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Taifa (CHADEMA) Freeman Mbowe amepinga kauli hiyo.
Mbowe alisema kuwa ikiwa jeshi la polisi litaamua kuwakataza kuendesha mafunzo hayo kwa vijana wao, ambayo alisema yanatolewa mchana wataamua kutoa mafunzo usiku.

Kiongozi huyo alitoa kauli hiyo jana wakati akifunga mafunzo ya vijana wapatao 200 katika wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu, ambapo alibainisha kuwa mafunzo hayo yanatolewa kwa vijana wao ni juu ya uzalendo.


Aliongeza kuwa kitendo cha tamko la viongozi wa jeshi hilo, ni woga wa chama Cha Mapinduzi pamoja na wivu kwa Chadema, kuona wanaungwa mkono na mamia ya vijana nchi nzima kupata mafunzo hayo.
 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527