YANGA TAYARI NI WAFALME!!,MATOKEO MCHEZO WA LEO YAKO HAPA







leooo
Yanga Bingwa 2015/2016!! Hizi ni baadhi ya headlines kwenye kurasa za michezo.. haikumaanisha kwamba matokeo ya mwisho yalikuwa yameamua hvyo, ila wanaspoti walipiga hesabu ya pointi ambazo tayari YANGA walikuwa wamejikusanyia mpaka mechi yao ya mwisho, hii ya leo ambayo Yanga wamekutana na Polisi Morogoro tayari imetoa matokeo.

Yanga imefikisha jumla ya pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote inayoshiriki ligi kuu msimu huu, kwa matokeo hayo basi Yanga wanakuwa mabingwa wa Ligi hiyo.

Mechi hiyo kati ya Yanga na Polisi Moro ilikuwa ikipigwa katika Uwanja wa Taifa Dar.. mechi imekamilika kwa Yanga kutoka kifua mbele kwa goli 4-1.

Hamis Tambwe leo aliweza kuing’arisha Yanga baada ya kupachika magoli matatu ambapo goli la kwanza alifunga dakika ya 40 kufuatia krosi ya Saimon Msuva, goli la pili alilifunga dakika ya 53 na goli la mwisho alifunga baada ya kupokea cross kutoka kwa Mrisho Ngassa.

Msuva alikamilisha idadi ya mabao kwa kupiga bao la nne ambapo baadae dakika ya 83 Polisi walishinda bao la kufutia machozi kupitia kwa Bantu Admini aliyepiga shuti kali akiwa nje ya 18.

Ligi kuu Tanzania Bara inatarajiwa kukamilika mwisho wa wiki katika mechi za kukamilisha ratiba ya ligi hiyo kwa msimu huu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527