Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JAMAA ALIYETEKA MWANAFUNZI WA KIKE ,AZUA BALAA JINGINE POLISI!!

large_smoker-tax-cigarette
Ukishakuwa chini ya ulinzi kituo cha Polisi kuna vitu ambavyo hauko huru kufanya kwa sababu tu ya sheria za maeneo hayo.. hii stori iko kwenye headlines za vyombo vya Kenya, mitandao imeandika pia.


Inamhusu Henry Magee, alikuwa anashikiliwa na Polisi kwa kesi ya kumteka mwanafunzi wa kike.

Kesi ambayo iliongezeka kwa huyu bwana ilikuwa ni ishu ya kuvuta sigara akiwa selo.. akafikishwa tena Mahakamani na kutozwa faini ya Sh 15,000 za Kenya katika Mahakama ya Eldoret baada ya kukubali kufanya kosa  hilo.

Mtuhumiwa huyo Henry Magee alitozwa faini hiyo na Hakimu Tom Olando, ambae amesema alisikia harufu ya moshi wa sigara akiwa kwenye chumba chake cha kusikilizia kesi, chumba hicho kiko jirani na selo ambayo Henry alikuwa amefungiwa.

Jamaa alipewa nafasi ya kujitetea; “Ni kweli nilifanya makosa ambayo yametajwa dhidi yangu lakini ni kwa sababu ya mazoea ya kutumia sigara,”– Magee.


Kitu ambacho nimejiuliza ni kwamba watu wengi akishakua yuko selo anakuwa na uoga hivi, sasa huyu jamaa kapataje ujasiri wa kuvuta sigara kabisa ndani ya chumba cha jela !!

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com