Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Inatisha Sana!! WANAFUNZI 6 WALIOKUFA KWA RADI NA MWALIMU WAO WAKIWA DARASANI WAZIKWA HUKO KIGOMA

Mkuu wa mkoa wa kigoma Luten Kanal Mstaafu Issa Machibya  amewaongoza mamia ya wakazi wa manispaa ya Kigoma Ujiji  kuaga miili ya watu wanane wakiwemo wanafunzi  sita wa darasa la kwanza katika shule ya msingi ya Kibirizi Mjini Kigoma wali fariki dunia jana baada ya kupigwa na radi kufuatia mvua iliyonyesha kwa takribani masaa matatu.

Majonzi yalitawala shughuli hiyo  hasa baada ya miili hiyo kupokelewa katika viwanja  vya  shule ya msingi Kibirizi kabla ya ndugu kukabidhiwa tayari kwa maziko huku mwili wa Mwalim Elieza Mbwambo ukisafirishwa kwenda Moshi kwa maziko .
 
 Akitoa salamu za rambirambi mkuu wa mkoa wa Kigoma Luten Kanal Mstaafu Issa Machibya amewataka wafiwa na wananchi kuchukulia  tatizo hilo kama ni tukio la ajali ya kawaida na kwamba msiba huo ni mzito.
 
Kwa upande wao viongozi wa dini Sheikh Moshi Guoguo kutoka Bakwata na mchungaji Emmanuel Mtoi wa kanisa la KKKT wakitoa mawaidha katika msiba huo, 
wamewataka waumini wa dini mbalimbali kujiandaa kwa kuwa kila mwanadamu ataonja mauti  kwa wakati wake na kwamba imani za kishirikina zisihusishwe katika msiba huo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com