Angalia Picha -CHADEMA(Ukawa) NOMA SANA!! WAFANYA MAAJABU SHINYANGA MJINI,LEMA,KATAMBI WAFANYA KWELI!!

Hapa ni katika viwanja vya Mahakama ya Mwanzo Nguzo Nane mjini Shinyanga ambapo leo jioni mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema pamoja na mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) taifa Patrobas Katambi wamehutubia maelfu ya wakazi wa Shinyanga na kutoa elimu ya uraia.Pamoja na mambo mengine Gobless Lema amewataka Watanzania kubadilika na kuacha tabia ya Uoga katika kufanya maamuzi magumu ikiwemo kuwaondoa madarakani viongozi wasio waadilifu-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(BAVICHA) taifa Patrobas Katambi akizungumza katika mkutano huo ambapo alitangaza rasmi nia kugombea ubunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Kupitia UKAWA katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
Katambi alisema yeye ni mzaliwa wa Shinyanga hivyo atakomaa katika jimbo la Shinyanga Mjini kuhakikisha anagombea ubunge ili kuondoa uongozi wa Chama Cha Mapinduzi ambao umekuwa ukifanya ubadhirifu wa fedha na kutowaletea maendeleo wananchi.Baada ya kutangaza nia hiyo Umati wa watu ukapiga kelele nyingi wakiashiria kuwa walikuwa wanamsubiri kwa hamu atamke kuwa atagombea kwani anaonekana kuwafaa wakazi wa Shinyanga
“Mimi ni mtu wa Shinyanga,Natangaza rasmi kuwa nitagombea ubunge katika jimbo la Shinyanga Mjini,uwezo ninao na nia ninayo,naungana na watangaza nia wengine waliotangulia,naomba ushirikiano tu,kama jina langu litapitishwa tutafanya mambo makubwa katika jimbo hili, kwani najiamini na najua ninachokifanya,na siku zote mti wenye matunda ndiyo unaopigwa mawe,mimi naamini katika haki zaidi na kufuata sheria za nchi,mwaka huu lazima kieleweke”,alieleza Katambi.
Wakazi wa Shinyanga wakifuatilia kilichokuwa kinajiri eneo la mkutano.“Sijajipitisha kugombea,bali nitafuata taratibu za Chama changu,nitaandika barua kupeleka jina langu ili kusimikwa kuwa mgombea wa ubunge na endapo atapitishwa mtu mwingine zaidi yangu,tutamuunga mkono kwani chama chetu ni cha Umoja na tunafanya kazi moja ya kuleta ukombozi kwa wananchi”,alieleza  Katambi.

Kushoto ni Mtangaza nia ya Ubunge Shinyanga Mjini  Patrobas Katambi akiwa na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema ambaye naye alijigamba kuwania ubunge katika jimbo lake.

Wakazi wa Shinyanga wakifurahia baada ya kusikia kuwa Bwana Patrobas Katambi kuwa atawania ubunge katika jimbo la Shinyanga mjini ambalo sasa linaongozwa na mbunge wa CCM ndugu Stephen Masele
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema akizungumza na wakazi wa Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine amewataka watanzania Kumpuuza kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe kwa madai kuwa amepewa pesa na CCM ili azunguke nchi nzima kuvuruga Chadema(UKAWA) lakini akasisitiza kuwa Kamwe Hataweza kwani wameshajua anachokifanya ndiyo maana kwenye mikutano yake hathubutu kuisema vibaya CHADEMA na maeneo aliyothubutu wananchi wamekuwa wakimzomea.

Godbless Lema pia alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama nchini kufanya kazi kwa kuzingatia sheria za nchi badala ya kupendelea chama Tawala.

Mbunge Lema pia alisema  Kitendo cha Zitto Kabwe kujitangaza kuwa ni Mzalendo ni Unafiki Mtupu kwani Uzalendo haupimwi kwa Umaskini kwani hakuna mtu anayependa kuwa maskini kila mtu anapenda kuwa na maisha mazuri.

Mkutano unaendelea-Lema pia alidai kuwa Matatizo mengi yaliyopo nchini Tanzania siyo CCM bali ni Uoga wa Watanzania wenyewe kufanya maamuzi magumu

Jukwaa kuu wakifuatilia kilichokuwa kinajiri kwenye mkutano

Mkutano unaendelea

Jukwaa kuu wakifuatilia hotuba ya mheshimiwa Godbless Lema

Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la mkutano

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post