Katika pitapita zake mjini Shinyanga kamera zetu zikanasa hili daraja lililopo katika barabara ya Magadula inayoelekea kwenye gereji ya Mohamed Trans kama wenyeji wa eneo hilo wanavyoiita,kamera zetu zikaona likiwa limewekewa kingo ya miti na kamba ili kuwasaidia watumiaji wa barabara hiyo wasitumbukie kwenye mto unaopita katika daraja hilo,ambapo hivi karibuni gari ndogo ilitumbukia huku kukiwa na taarifa kuwa watumiaji wengi wa barabara wakiwemo waendesha baiskeli na watembea kwa miguu wamekuwa wakitumbukia na kuondoka kimya kimya.
![]() |
Pengine labda kamba hizo na miti iliyowekwa itawasaidia watumiaji wa barabara hiyo kutumbukia kwenye daraja hilo,lakini mtandao huu hauna uhakika sana kwa hilo |
![]() |
Muonekano wa daraja hilo lisilokuwa na kingo kwa mbali,ambapo kama ni mgeni wa barabara hiyo kutumbukia darajani ni jambo la kawaida hasa nyakati za usiku |
![]() | ||
Ndiyo ukingo wa daraja ambao uliwekwa ziku chache zilizopita kutokana na ujio wa rais Jakaya Kikwete akihudhuria shughuli ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa askofu wa jimbo katoliki la Shinyanga Liberatus Sangu ambapo msafara wake ulipita hapoBOFYA MANENO HAYA KUONA TUKIO LA GARI KUTUMBUKIA KWENYE MTO |
Social Plugin