ANGALIA PICHA- VIJANA WA KANISA KUBWA LA KKKT SHINYANGA WAFANYA TUKIO KUBWA KWENYE KITUO CHA WALEMAVU WA NGOZI ALBINO CHA BUHANGIJA!!
Sunday, April 19, 2015
Hapa ni katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa
ngozi(Albino) wasiosikia na wasioona cha Buhangija Jumuishi kilichopo katika manispaa ya
Shinyanga,ambapo leo Jumapili April 19,2015 Kkundi cha vijana kutoka Idara ya Vijana wa Kanisa la KKKT
kanisa Kuu Ebenezer Shinyanga Mjini wametembelea kituo hicho kisha kuendesha
maombi na baadaye kutoa msaada wa chakula na mahitaji mengine ya kibinadamu
vyote vikiwa na thamani ya shilingi laki 6-picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Vijana hao wa KKKT kanisa Ebenezer Shinyanga Mjini wakiongozwa na mwenyekiti wao bwana Ombeni Kweka wametoa msaada wa mafuta ya kupikia ndoo 6,maharage kilo 50,mchele kilo 100,dawa za binadamu zenye thamani ya shilingi laki moja,pakti 4 za biskuti,kalamu 150,pipi,nguo na sabuni.Aliyesimama kulia ni mlezi/mkuu wa kituo cha Buhangija Peter Ajali akiwakaribisha vijana hao
Mwenyekiti wa kikundi cha Idara ya Vijana KKKT kanisa Kuu Enezener Ombeni
Kweka akizungumza katika kituo cha Buhangija ambapo alisema vitendo vya ukatili
wanaotendewa albino vinamuudhi mwenyezi mungu hivyo kuitaka serikali kuchukua
hatua kali dhidi ya wahusika wa vitendo hivyo vya kikatili ikiwa ni pamoja na
kuharakisha kesi zao ili vitendo hivyo visijirudie.
Mwenyekiti
wa maombi idara ya Vijana wa KKKT kanisa kuu la Ebenezer Shinyanga mjini Astiye Mwaipopo akiongoza maombi maalum katika kituo cha Buhangija mjini Shinyanga.
Maombi yanaendelea-Kituo cha Buhangija hivi sasa kina watoto wenye ulemavu wa
ngozi 284,wasioona 40 na wasiosikia 64 huku idadi ya albino ikiongezeka kila
siku kutoka maeneo ya ndani na nje ya manispaa ya Shinyanga kwa hofu ya kuuawa.
Mwenyekiti
wa maombi idara ya Vijana wa KKKT kanisa kuu la Ebenezer Shinyanga mjini Astiye Mwaipopoaliwataka watoto wenye ulemavu kutokata tama ili kutimiza ndoto zao kwani wapo
watu wenye albinism wamefanikiwa katika maisha.
Maombi yanaendelea-wa kwanza kushoto ni bwana Penny Nkya kutoka idara ya Vijana wa KKKT kanisa
kuu Ebenezer Shinyanga mjini akifuatilia kwa ukaribu zaidi kilichokuwa
kinaendelea
Katibu
wa Vijana KKKT Ebenezer Kanisa Kuu Hoyce Mramu akinong’ona jambo na Mdeakonia
wa kanisa la KKKT kanisa kuu Ebenezer Shinyanga Mjini Edna Shoo(wa kwanza kushoto) katika kituo cha
Buhangija.
Vijana wa KKKT kanisa kuuu Ebenezer Shinyanga mjini wakiwa Buhangija
Katibu
wa Vijana KKKT Ebenezer Kanisa Kuu Hoyce Mramu akionesha baadhi ya vitu walivyopelekwa kwa ajili ya watoto wenye ulemavu Buhangija
Katibu
wa Vijana KKKT Ebenezer Kanisa Kuu Hoyce Mramu akimkabidhi mtoto mwenye ulemavu wa ngozi boksi la Kalamu
Katibu
wa Vijana KKKT Ebenezer Kanisa Kuu Hoyce Mramu akishikana mkono na mtoto mwenye ulemavu wakati akikabidhi msaada kwa niaba ya wenzake.
Makabidhiano yanaendelea-Mkuu wa kituo cha Buhangija Jumuishi Mwalimu Peter Ajali
akizungumza wakati wa kupokea msaada kutoka kwa vijana wa KKKT ambapo pamoja na
kuwashukuru kwa kuwafikia watoto hao pia hakusita kuiomba jamii kuendelea
kukisaidia kituo hicho kinachokabiliwa na tatizo la
Chakula,Vitanda,Magodoro,Masweta na dawa za binadamu.
Kijana
Hassan Hamis akishukuru kupokea msaada kutoka kwa vijana wa kanisa la KKKT ,kwa
niaba ya watoto wenye ulemavu katika kituo cha Buhangija.
Hivi
sasa kituo cha Buhangija kina watoto wenye ulemavu wa ngozi (albino) zaidi ya
280,wasiosikia 64 na wasioona 40,na idadi ya albino inaongezeka kila kukicha
ambapo hadi April 19,2015 watoto albino wapo 284.
Kijana Hassan Hamis akitoa wito kwa wananchi wenye mapenzi mema kuendelea kutoa msaada kwa watoto wa Buhangija Jumuishi
Mkuu wa kituo cha Buhangija Peter Ajali akiwa amebeba mfuko wa pipi
Mmoja wa vijana kutoka kanisa la KKKT akiwa amebeba mtoto katika kituo cha Buhangija
Vijana wa kanisa la KKKT Ebenezer wakigawa pipi kwa watoto
katika kituo cha Buhangija
Vijana wa KKKT wakiendelea kugawa pipi kwa watoto-picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin