Hatari!! WANAWAKE WA KIMASAI WAENDELEA KULALA PORINI BAADA YA WAUME ZAO KUKIMBIA MIJI YAO

Wanawake wa Kimasai katika kijiji cha Mabwegere wilayani Kilosa mkoani Morogoro wamelalamikia kuishi maisha magumu baada ya  wanaume kukimbia makazi na kuwaachia mzigo wa kulea familia   kufuatia mapigano yaliosababisha mauaji ambapo wanawake wengine wamelalamikia kujifungulia majumbani kutokana na kushindwa kumudu gharama za kwenda katika vituo vya afya.
  

Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia baadhi ya nyumba zimefungwa ambapo wakizungumza wakiwa maporini wanawake hao wamesema baadhi ya watu wameyakimbia makazi yao kutokana na kuishi kwa hofu ambapo wamesema migogoro hiyo ya ardhi inawaathiri wanawake na watoto zaidi kwani wanaume wamekimbia na kuwaachia mzigo wa kulea familia huku wengine wakikosa msaada na wengine wakishindwa kumudu gharama za matibabu na hivyo kuomba serikali kusimamia kumaliza migogoro hiyo.
 
Naye mwenyekiti wa kijiji cha Mabwegere Mika Kashu amekiri baadhi ya wanawake kuishi katika mazingira magumu ambapo amesema waliohusika na mauaji hayo wanafahamika na hivyo kuomba serikali iwachukulie hatua kwani oparation ya kamatama imesababisha hofu na wanaume kulazimika kukimbia kijiji.
 
Afisa utawala wa wilaya ya Kilosa Hilary Sagala akizungumza na  kwa anjia ya simu amesema jeshi la polisi limeimarisha ulinzi katika eneo la Mabwegere na kuhusu wafugaji kukimbia makazi amesema hakuna sababu ya watu kukimbia makazi kama hawakuhusika na tukio la lililosababisha mauaji na kuwataka wananchi kurejea katika makazi yao  waendelee na shughulizao kama kawaida.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527