Serikali
imeshauriwa kutekeleza kwa uangalifu mkubwa adhima yake ya kupambana na
waganga wa jadi wanaojihusisha na upigaji ramli zinazodaiwa ni chanzo
cha mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albinism) kwa vile hatua hiyo
inaweza kusababisha madhara makubwa kwa taifa.
Ushauri
huo umetolewa na mmoja wa wazee maarufu mjini Shinyanga, Iddi Juma ambapo amesema serikali haipaswi
kukurupuka katika kushughulikia suala la waganga wa jadi kwa vile baadhi
yao wana umuhimu mkubwa kwa jamii na wamekuwepo nchini tangu enzi na
enzi.
"Hivi
kweli kuna tiba yoyote ya majini au mapepo machafu katika hospitali
zetu nchini? wanaopatwa na matatizo haya mara nyingi tunaona
wanakimbizwa kwa waganga wa jadi, ndiyo wataalamu wa kuyatibu, na huko
ni lazima mganga afanye mambo yake ili kubaini yametokea wapi, sasa
tukiwakamata wenye matatizo haya watatibiwa wapi?" alihoji Juma.