HAYA NDIYO MAAJABU 10 USIYOYAJUA KUHUSU MOYO WAKO

 

1. Kwa siku moyo huzalisha nguvu ambayo ina uwezo wa kusukuma lori kwa umbali wa maili 20.


2. Katika muda wote wa uhai wa mwanadamu moyo husukuma karibu mapipa milioni 1.5 ya damu ambayo ni sawa na kujaza matenki 200 ya treni.


3. Seli za moyo huanza kupiga mapema zaidi kuanzia wiki ya nne mtoto awapo tumboni.

4. Nyangumi ajulikanae kwa rangi yake ya bluu (Blue whale) ana moyo mkubwa wenye uzito upatao kilogramu 680.

5. Mshituko wa moyo wakati wa kufanya mapenzi ni kiasi kidogo sana na huwatokea sana wanaume pindi watokapo nje ya ndoa.

6. Furaha, kukosa wasiwasi, mazoezi na mlo kamili husaidia kuwa na moyo wenye afya bora.

7. Binadamu anakuwa katika hari ya kupata mshituko wa moyo siku ya jumatatu asubuhi zaidi ya siku zingine zote.

8. Moyo unauwezo wa kuendelea kudunda hata ukiwa nje mwili wa unachohitaji wenyewe ni hewa ya oksijeni tu.

9. Moyo wa mwanamke hudunda haraka zaidi ya moyo wa mwanaume.

10. Kicheko hupelekea kiasi cha asilimia 20 ya damu kuzunguka mwilini na kukufanya uongeze siku za kuishi kwa kutoa msaada zaidi kwenye moyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527