Mwanamme mmoja aliyejulikana kwa jina la Makoye Malungu(65) mkazi wa kijiji cha Mwakadimu wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu amefariki dunia baada ya kutumbukia katika dimbwi la maji baada ya kuteleza wakati akitokea kwenye klabu ya pombe za kienyeji.
Kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu Charles Mkumbo amesema tukio hilo limetokea juzi baada ya Malungu kunywa pombe za kienyeji nyingi kupindukia na akiwa njiani,aliteleza na kutumbukia katika dimbwi hilo na kufariki dunia.
Na Anceth Nyahore-Simiyu
Social Plugin