
Mkazi wa kijiji cha Mwamigongwa kata ya Malili tarafa ya Kivukoni wilaya ya Busega mkoani Simiyu,Dotto Bahame(32) ameuawa kwa kuchomwa kisu shingoni katika ugomvi wa kuwania fedha baada ya kucheza kamari.
Kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu Charles Mkumbo amesema tukio hilo limetokea Januari 6,2015 saa 12 jioni kijijini hapo baada ya kundi la watu waliokuwa wakicheza kamari,kutoelewana juu ya mapato waliyoyapata na kusababisha ugomvi amabo unasadikiwa mmoja wao alichomoa kisu na kumchoma shingoni Bahame ba kufariki dunia papo hapo.
Alisema licha ya kisu kilichotumika kwa mauaji hayo kupatikana lakini bado mhusika wa tukio hajafahamika.
Mkumbo alisema mtuhumiwa wa tukio hilo hajafahamika na wanaendelea kumsaka.
Na Anceth Nyahore-Simiyu
Social Plugin